Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Sospeter M, MD
Jumatatu, 16 Agosti 2021
Panado kwa watoto
Panado, dawa yenye kiini cha acetaminophen ni maarufu sana kutuliza maumivu ya jeraha, tumbo, sikio na homa kwa watoto. Kama haipatikani katika mazingira yako, tumia ibuprofen kama mbadala.
Fomu mbalimbali za panado
Kuna fomu mbalimbali za panado zinazopatikana madukani, fomu ya maji hutumika mara nyingi, hata hivyo kuna fomu nyingine za vidonge vya kunywa na vidonge vya kuweka ndani ya njia haja kubwa kwa watoto wanaoshindwa kunywa dawa kwa sababu mbalimbali.
Fomu gani ya panado itumike kwa watoto?
Watoto wanaweza tumia fomu mbalimbali za panado kulingana na umwi wao
Mtoto kuanzia umri wa miezi miwili inafaa atumie panado ya maji hata hivyo anaweza kutumia vidonge maalumu vya kuweka njia ya haja kubwa
Mtoto mwenye umri kuanzia miezi sita na kuendelea anaweza tumia panado ya kidonge
Mbadala wa Panadol kwa watoto
Kama huwezi pata panado chaguzi ya kwanza, unaweza tumia dawa zingine za maumivu ili kushusha homa au kutibu maumivu ambazo ni;
Ibuprofen
Aspirini
Dawa ya ibuprofen na Aspirini kwa watoto
Inaweza tumika kama mbadala wa panado kwenye matibabu ya homa na maumivu kwa mtoto haswa aliye umri kuanzia miezi mitatu na kuendelea, hata hivyo isitumike kwa watoto wenye pumu ya kifua
Onyo la matumizi ya aspirini kwa watoto
Aspirini inashauriwa itumike watoto wenye umri zaidi ya miaka mitatu tu kwa kuwa huhusianishwa na sindromu ya reye’s( Ini na Ubongo huvimba) kutokana na matumizi ya aspirini haswa kwa watoto chini ya miaka miwili na wenye maambukizi ya kirusi cha tetekuwanga au mafua. Licha ya hofu ya kupata sindromu ya reye's, aspirini haipaswi kutumiwa na watoto chini ya miaka mitatu na wale wenye maambukizi ya kirusi cha mafua au tetekuwanga au wale wanaokaribia kupona maambukizi hayo.
Madhara ya panado kwa mtoto
Licha ya panado kuwa salama kama itatumika kwa dozi sahihi, dawa hii inaweza kusababisha mzio mkubwa wa anafailaksia.
Mambo muhimu ya kukumbuka
Panado haitibu chanzo cha ugonjwa hivyo unapompa mtoto kwa ajili ya kushusha homa, hakikisha unampeleka kituo cha afya kufanyiwa uchunguzi .
Vidonge na maji ya panado huwa na nguvu mbalimbali kutegemea nguvu aliyoiweka mtengeneza dawa( uzito wa kiini cha dawa), hivyo kuwa makini unapompa dawa mtoto ili kuzuia kumpa mtoto dozi kubwa zaidi yenye madhara kutokana na mazoea
Baada ya kutumia dawa, mtoto atanza kupata nafuu baada ya dakika 30 kama ametumia kidonge na hadi dakika 60 kama ametumia panado ya kuweka kwenye njia ya haja kubwa
Usimpe mtoto dawa nyingine ya maumivu yenye panado ili kuzuia kupata dozi kubwa. Hata hivyo hairuhusiwi kumpa dawa zaidi ya aina moja ya maumivu isipokuwa endapo umeshauriwa na daktari wako
Ingawa Panado ni dawa inayotumika kila siku, inaweza kuharibu ini na kusababisha kifo endapo itatumiwa bila kuzingatia dozi sahihi
Panado haipaswi kutumika zaidi ya siku tatu kwa mtoto isipokuwa endapo umeshauriwa na daktari wako na lazima kuwe na sababu
Dozi ya panado hutumika kila baada ya masaa sita hadi 8
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
7 Oktoba 2021 04:48:24
Rejea za mada hii:
1. Paracetamol for children. https://www.nhs.uk/medicines/paracetamol-for-children/. Imechukuliwa 16.08.2021
2. Medications for children: a guide. https://raisingchildren.net.au/guides/a-z-health-reference/medications. Imechukuliwa 16.08.2021
3. Reyes syndrome. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/reyes-syndrome/symptoms-causes/syc-20377255#. Imechukuliwa 16.08.2021
4. Maurizio de Martin, et al.Recent Advances in Pediatric Use of Oral Paracetamol in Fever and Pain Management. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4676765/. Imechukuliwa 16.08.2021
5. Dipak J. Kanabar, et al.A clinical and safety review of paracetamol and ibuprofen in children. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5306275/. Imechukuliwa 16.08.2021
6. N Cranswick, et al.Paracetamol efficacy and safety in children: the first 40 years. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/11319581/. Imechukuliwa 16.08.2021