top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Helen L, M.D

Jumanne, 2 Februari 2021

Punguza kupigwa na mionzi ya simu isiyo ya lazima kwa usalama wa afya yako

Punguza kupigwa na mionzi ya simu isiyo ya lazima kwa usalama wa afya yako

Usiongee nayo kwa muda mrefu au wakati wa kuchaji, kulala karibu, kuhifadhi maeneo ya kifuani au kuweka karibu na sehemu za siri simu yako ya mkononi. Ukifanya hivi utaepuka kupigwa na mionzi isiyoya lazima inayozalishwa na simu yako. Fanya hivi kujilinda na hatari ya kupata saratani


Matumizi salama ya simu ya mkononi


Watu wengi duniani kwa sasa wanatumia simu kurahisisha mawasiliano ya kimahusiano na kibiashara. Ongezeko la simu za kisasa zenye jina simu janja au ‘smartphone’ sokoni ni kubwa sana na mamlaka mbalimbali za kiafya zimeanza kuangalia madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya simu hizo.


Baadhi ya tafiti zilizofanyika zimeonyesha kuwa, simu ni moja ya kihatarishi cha kupata uvimbe ambao unaoweza kuwa wa kawaida au saratani haswa maeneo ya ubongo na masikio.


Tafiti zingine pia zinaeleza kuwa endapo simu itawekwa karibu na maeneo ya sehemu za siri, husababisha uharibifu wa


 • Kubadilika kwa maumbile ya mbegu za kiume na mayai

 • Mbegu za kiume kupunguza uwezo wake wa kukimbia

 • Kubadilika kwa vinasaba vya mbegu za kiume na mayai


Mabadiliko haya huweza kusababisha ugumba, kutoka kwa mimba au kupata watoto wenye madhaifu.


Tafiti nyingi zilizofanyika, zinaita kufanyika kwa tafiti nyingine ili kufahamu zaidi kuhusu madhara ya simu kwa binadamu.


Mambo ya kuzingatia kuhusu simu


Licha ya kuwepo kwa simu nyingi sana duniani, zipo simu ambazo zina uwezo wa kutoa mionzi mingi kuliko simu zingine. Kuna kiwango cha mionzi kinachotolewa na simu husemekana kuwa ni salama, kiwango hiki hutofautiana katika nchi na nchi na huitwa kwa jina la ‘Specific absorption rate’ au kwa kifupi SAR. Licha ya baadhi ya nchi kuwa na kiwango chake, usalama wa kiwango hiko kinachokubalika bado haufahamiki, tafiti zinahitajika kufanyika zaidi ili kutoa SAR ambayo itatumika kama rejea ya kiwango salama.


Nchi nyingi za kiafrika bado hazina kiwango chake kinachoonekana kuwa ni salama, licha ya kununua simu kutoka mataifa mbalimbali, na pia kutumia simu ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kuuwa barani Afrika


Nchi ambazo zimejichaguliwa viwango vya mionzi ya simu, zimepiga marufuku utumiaji wa simu zinazotoa mionzi zaidi ya kiwango kinachotakiwa katika nchi zao.


Mfano


 • Ujerumani- simu zenye SAR 0.6 au pungufu zinakubalika kutumika

 • Marekani – simu zenye SAR 1.6 au pungufu tu zinakubalika kutumika

 • Nchi za muungano wa Ulaya – Simu zenye SAR chini ya 2 zinakubalika kutumika

 • India- simu zenye SAR chini ya 1.6 zinakubalika kutumika


Baadhi ya simu zenye SAR kubwa


Jifunze kupitia linki hii kuhusu simu zenye SAR kubwa na na zipi zenye SAR ndogo ili kuchangua aina gani ya simu unaweza kutumia.


Ushauri kutoka kwenye tafiti


Unashauriwa kuhifadhi simu yako katika maeneo ambayo angalau yana usalama kiafya. Pia unashauriwa kutumia simu ambazo zinatoa mionzi kidogo yaani zenye SAR ndogo. Epuka kutumia simu ambazo zimeharibika au ambazo hazina kiwango.


Hatua za kufanya kupunguza mionzi


 • Fanya mambo yafuatayo ili kupunguza hatari ya kupatwa na mionzi mingi ya simu

 • Usiongee na simu kwa muda mrefu

 • Usiongee na simu mara nyingi kwa siku

 • Tumia simu ya mkononi tu endapo simu ya mezani haipatikani

 • Tumia kifaa kinachoongeza umbali kutoka kwenye simu yako dhidi ya masikio au kichwa mfano ‘earphone’ na ‘headphone’

 • Usilale karibu na simu au zima simu kabla ya kulala


Usitumie simu wakati ipo chaji


 • Unapokuwa umekaa weka simu mbali nawe badala ya kuishika au kuiacha mwilini mwako •Ukiwa unatembea na simu, iweke kwenye pochi kisha beba mkononi mwako badala ya kuweka kwenye kifua au mifuko ya suruali yako

 • Usitumie simu ambayo haitoi sauti vema au kuwa ya moto wakati wa matumizi

 • Simu inapokuwa yamoto wakati wa kutumia, acha kuitumia mpaka ipoe

 • Usitumie simu yenye SAR kubwa

 • Usiongee na simu ya mkononi wakati umewasha data

 • Usiweke wireless kwenye simu kutumia kwenye kompyuta yako badala yake unaweza kutumia njia ya USB tethering

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:41:55

Rejea za mada hii:

1.Martha S. Linet, et al. Cellular (Mobile) Telephone Use and Cancer Risk. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3855294/#. Imechukuliwa 01.02.2021

2.Jitendra Kumar Meena, et al. Mobile phone use and possible cancer risk: Current perspectives in India. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4922278/. Imechukuliwa 01.02.2021

3.International Commission on Non-Ionizing Radiation Protection (ICNIRP). Guidelines for limiting exposure to time-varying electric, magnetic, and electromagnetic fields (up to 300 GHz). Health Phys 1998;74:494–522.c Basic guidelines paper by ICNIRP, a non-governmental organization consisting of about a dozen experts. Basis of these guidelines are immediate effects such as tissue heating.

4.National Radiological Protection Board. 1999. Advisory Group on Nonionising Radiation. Inapatikana: www.nrpb.org.uk/Advice/Nir-is4.htm.

5.MOBILE PHONE USE AND CANCER. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1763636/pdf/v061p00560.pdf. Imechukuliwa 01.02.2021

6.Statista. The Phones Emitting the Least Radiation. https://www.statista.com/chart/12841/the-phones-emitting-the-least-radiation/. Imechukuliwa 01.02.2021

7.Specific Absorption Rate (SAR) For Cell Phones: What It Means For You. https://www.fcc.gov/consumers/guides/specific-absorption-rate-sar-cell-phones-what-it-means-you#. Imechukuliwa 01.02.2021

8.WHO. https://www.who.int/health-topics/electromagnetic-fields. Imechukuliwa 01.02.2021

9. Igor Gorpinchenko, et al. The influence of direct mobile phone radiation on sperm quality. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4074720/. Imechukuliwa 01.02.2021

10.Chidiebere Emmanuel Okechukwu. Does the Use of Mobile Phone Affect Male Fertility? A Mini Review. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7727890/. Imechukuliwa 01.02.2021

11.Kavindra Kumar Kesari,et al. Radiations and male fertility. https://rbej.biomedcentral.com/articles/10.1186/s12958-018-0431-1. Imechukuliwa 01.02.2021

bottom of page