top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Helen L, M.D

Jumamosi, 6 Februari 2021

Salmonella typhi husababisha taifod

Salmonella typhi husababisha taifod

Salmonella typhi ni kimelea pekee anayesababisha taifodi kali kwa binadamu, kimelea huyu huweza fanya makazi na kuzaliana kwenye kibofu cha nyongo kwa muda mrefu hivyo kusababisha taifodi sugu. Endapo taifodi yako haiishi kwa matibabu, inawezekana una vimelea hao kwenye kibofu cha nyongo. Ukipata matibabu sahihi utapona na kuwakinga ndugu kupata maambukizi.


Vimelea wawili wanaosababisha taifodi


Kimelea salmonella typhi, husababisha taifodi kali kwa binadamu, ukilinganisha na vimelea wengine kama salmonella paratyphi. Kimelea huyu huhifadhiwa na kuishi kwenye matumbo ya binadamu, na hivyo husafirishwa kwa njia ya kinyesi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.


Endapo utakula chakula kilichoandaliwa na mtu mwenye vimelea vya taifodi, au kutumia maji yaliyochangamana na kinyesi chenye vimelea, unaweza kupata maambukizi hayo. Watu walio na kimelea huyu kwenye kibofu cha nyongo, hupata taifod sugu isiyopona kirahisi. Mtu mwenye vimelea vya taifodi kwenye kibofu cha nyongo, anaweza kuambukiza watu wengi katika kipindi cha mwaka au zaidi.


Mgonjwa mwenye taifodi sugu anaweza kuonyesha au kutoonyesha dalili zozote zile. Taifodi sugu huhitaji matibabu maalumu na ya muda mrefu ili kuondoa vimelea wanaoishi ndani ya kibofu cha nyongo na matumbo.


Dalili za taifodi


Dalili za taifodi hujumuisha;


 • Homa

 • Maumivu ya kichwa

 • Kukosa hamu ya kula

 • Maumivu yamaungio ya mwili

 • Maumivu ya tumbo

 • Maumivu tumbo likishikwa

 • Kuharisha damu kwa taifodi kali

 • Kupata madoa kwenye ngozi kwa taifodi kali


Namna ya kujikinga na taifod


 • Kunywa maji safi yaliyochemshwa au kutiwa chlorine au kutakaswa

 • Kinyesi na maji ya kinyesi yanabidi kutunzwa kwa usalama ili yasikutane na chakula au maji anayotumia binadamu

 • Watu wenye taifodi sugu, wanatakiwa wasijihusishe na uandaaji wa chakula kwa ajili ya wengine haswa kwa wagonjwa na watoto mpaka watakapothibitishwa kwa vipimo kwamba hawana vimelea hao kwenye kinyesi.

 • Usile vyakula ambavyo havijapikwa vema mfano kachumbari, mboga za majani au matunda. Tumia vinegar kutengeneza kachumbari ili kuua vimelea.

 • Kula vyakula vilivyopikwa vema na bado ni vya moto au vinatoa mvuke wa joto

 • Endapo unataka kula vyakula ambavyo havijapikwa, tumia maji salama yaliyochemshwa au kuwekwa chlorine ili kuosha matunda na mboga za majani kabla ya kula au kutengeneza kachumbari

 • Nawa mikono yako kwa maji safi na sabuni kabla ya kula

 • Pata chanjo

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:41:55

Rejea za mada hii:

1.Typhoid Fever . https://www.msdmanuals.com/professional/infectious-diseases/gram-negative-bacilli/typhoid-fever. Imechukuliwa 06.02.2021

2.Ryan ET. Epidemiology, microbiology, clinical manifestations, and diagnosis of typhoid fever. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 06.02.2021

3.Centers for Disease Control and Prevention. Typhoid fever.https://www.cdc.gov/typhoid-fever/index.html. Imechukuliwa 06.02.2021

4.Victoria state government. Typhoid and paratyphoid. https://www2.health.vic.gov.au/public-health/infectious-diseases/disease-information-advice/typhoid-and-paratyphoid. Imechukuliwa 06.02.2021

5.WHO. Immunization, Vaccines and Biologicalshttps://www.who.int/teams/immunization-vaccines-and-biologicals/diseases/typhoid. Imechukuliwa 06.02.2021

6.Centers for Disease Control and Prevention. Typhoid Fever and Paratyphoid Fever. https://www.who.int/teams/immunization-vaccines-and-biologicals/diseases/typhoid. Imechukuliwa 06.02.2021

7.S. L. Hoffman, et al. Effective treatment and prevention of typhoid fever. Updated. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2279614/. Imechukuliwa 06.02.2021

8.Malick M. Gibani, et al. Typhoid and paratyphoid fever: a call to action. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6319573/. Imechukuliwa 06.02.2021

bottom of page