top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Helen L, M.D

Alhamisi, 28 Januari 2021

Tabia ya kukufanya upate usingizi kwa wakati

Tabia ya kukufanya upate usingizi kwa wakati

Lala na amka muda uleule kila siku, zima taa kutengeneza giza na hakikisha hakuna kelele yoyote, zima na weka simu mbali na kitanda, usile mlo mkubwa wala kunywa kahawa au pombe masaa matatu kabla ya kulala na fanya mazoezi au kazi ya kukutoa jasho wakati wa mchana.


Hatua za kuzingatia ili upate usingizi kwa wakati


Tafiti zinaonyesha, kuna ongezeko kubwa la watu wenye madeni ya usingizi, hii inachangiwa na kukosa muda wa kulala unaoshauriwa kiafya. Madeni ya usingizi huchangia kupunguza ufanisi wa kimwili na kiakili.


Kujifunza namna nzuri ya kupata usingizi itasaidia kupunguza matatizo mengi yanayotokana na kukosa usingizi.


Mambo yafuatayo ili kupata usingizi kwa wakati


  • Lala na amka muda ule ule kila siku

  • Zima taa na hakikisha hakuna kelele sehemu unayolala kwa kuzima redio, TV n.k. Hakikisha pia wakati wa mchana unakuwa kwenye mwanga angavu.

  • Usinywe kahawa au kula mlo mkubwa wakati wa usiku haswa masaa matatu kabla hujalala

  • Usikae kwenye mwanga mkali au mwanga wenye rangi ya bluu wakati wa usiku

  • Usilale muda mrefu au bila mpangilio wakati wa mchana. Endapo unahitaji kulala wakati wa mchana hakikisha hulali zaidi ya lisaa moja au mawili

  • Ili kupata usingizi wakati unawaza vitu vingi, hesabu namba moja, mbili, tatu na kuendelea kwa kichwa bila kutamka mpaka utakapopata usingizi. Unaweza pia kufikiria kuhusu namna unavyovuta pumzi na kuitoa kutoka kwenye mfumo wa upumuaji

  • Tumia virutubisho au vyakula vinavyosemekana vinaleta usingizi

  • Pata tiba ya tatizo la msongo wa mawazo au magonjwa ya akili yanayosababisha kukosa usingizi

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:41:55

Rejea za mada hii:

1. CDC. Sleep. https://www.cdc.gov/sleep/index.html. Imechukuliwa 27.01.2021
2. CDC. Sleep and Sleep Disorders. https://www.cdc.gov/sleep/publications/factsheets.html. Imechukuliwa 27.01.2021
3. CDC. Short Sleep Duration Among US Adults. https://www.cdc.gov/sleep/data_statistics.html. Imechukuliwa 27.01.2021
4. Melatonin, the Hormone of Darkness: From Sleep Promotion to Ebola Treatment. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4334454/. Imechukuliwa 27.01.2021
5.Melatonin and Sleep. https://www.sleepfoundation.org/melatonin. Imechukuliwa 27.01.2021
6. Ingeborg M van Geijlswijk, etal. Evaluation of sleep, puberty and mental health in children with long-term melatonin treatment for chronic idiopathic childhood sleep onset insomnia. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/21340475/. Imechukuliwa 27.01.2021
7. T Shochat, etal. Melatonin--the key to the gate of sleep. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/9556097/. Imechukuliwa 27.01.2021

bottom of page