top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

Jumanne, 27 Julai 2021

Ufanisi wa dawa za mimba ya mapacha

Ufanisi wa dawa za mimba ya mapacha

Kutokana na ongezeko la matatizo ya uzazi kwa wanawake, kumepelekea matumizi makubwa ya dawa ya clomiphene citrate na dawa jamii ya gonadotrophin zinazoongeza hatari ya mimba ya mapacha au zaidi kwa asilimia 20 hadi 30 ya watumiaji. Je kila dawa ina ufanisi gani?


Dawa za kuongeza hatari ya mimba ya mapacha


Dawa za kuongeza uzazi huongeza hatari ya kupata mimba ya mapacha au zaidi, hufanya hivyo kwa kusisimua uzalishaji na utolewaji wa mayai mengi kwenye ovari.

Mayai mengi yanapozalishwa na kutolewa kwenye ovari, huongeza uwezekano mkubwa wa mayai hayo kuchavushwa kama yatakutana na manii katika siku za hatari.


Kuchavushwa kwa wakati mmoja wa mayai mawili au zaidi hupelekea kutokea kwa mapacha au zaidi na mara nyingi huwa mapacha ya watoto wasiofanana.


Dawa ya Clomiphene citrate na dawa za gonadotropin hutumika mara nyingi kuongeza uzazi kwa wanawake wanaopata shida ya kupata mtoto bila kuwa na shida kwenye mfumo wa uzazi. Matumizi ya dawa hizi huwa na madhara ya kuongeza hatari ya mimba ya mapacha. Utapata dawa hizi kwa kuandikiwa na daktari kwa kuwa ni dawa za cheti.


Mara unapokunywa clomifen na kuingia kwenye damu, dawa hii huenda moja kwa moja kuchochea uzalishaji wa homon zinazosababisha ovari kuzalisha mayai.


Dawa kichochea foliko (FSH) na kichochea utolewaji wa yai (LH) ni aina ya homoni jamii ya gonadotrophin, kwa kawaida hutengenezwa ndani ya ubongo na kazi yake ni kuamrisha ovari kuzalisha na kutoa yai moja kila mwezi.


Kuchoma dawa za FSH na LH hupelekea uzalishaji wa mayai mengi na huongeza hatari kupata mimba mapacha.


Je dawa za mimba ya mapacha zina ufanisi gani?


Matumizi ya clomofen yana ufanisi wa mimba ya mapacha au zaidi kwa asilimia 5 hadi 10, wakati huo matumizi ya dawa jamii ya gonadotrophin ina ufanisi wa asilimia 20 hadi 30 ya kupata mimba ya mapacha.


Hii inamaana kuwa kama wanawake 100 wakitumia clomifen citrate, ni wanawake wa 5 hadi 12 tu ndo watapata ujauzito wa mtoto zaidi ya mmoja (mapacha au zaidi ya mapacha) wakati huo kati ya wanawake 100 waliotumia FSH na LH, ni wanawake 20 hadi 30 tu watapata mimba ya mapacha au zaidi.


Dawa zote tatu huchukuliwa kuwa salama na ufanisi wa kazi yake ya awali. Hata hivyo katika matumizi ya dawa yoyote ile, kuna faida na hasara zake


Vihatarishi vingine vya kupata mimba ya mapacha


Vihatarishi vingine vya kupata mimba ya mapacha ni;


  • Kupata ujauzito kwenye umri zaidi ya miaka 37 au zaidi

  • Kuchelewa kupata ujauzito kwenye umri mdogo

  • Matumizi ya njia saidizi za kupata mtoto

  • Kuwa na historia ya mapacha kwenye familia ya upande wa kike


Madhara ya ujauzito wa zaidi ya mtoto mmoja


Ukilinganisha na ujauzito wa mtoto mmoja, zaidi ya nusu ya ujauzito wa mapacha huwa na hatari zifuatazo;


  • Mimba kutoka

  • Kujifungua kabla ya wakati

  • Kujifungua mtoto njiti

  • Mtoto kufia tumboni

  • Kujifungua mtoto ambaye hajakomaa viungo

  • Kufa kwa kichanga baada ya kujifungua

  • Mtindio wa ubongo kwa kichanga

  • Madhaifu ya kuzaliwa ya kimaumbile


Hatari za hapo juu huongezeka mara 10 hadi 20 kwa mimba ya watoto zaidi ya wawili ukilinganisha na mimba ya mtoto moja.


Madhara kwa mama


  • Shinikizo la juu la damu la ujauzito

  • Kunyofoka kwa kondo la nyuma

  • Kujifungua kwa upasuaji

  • Kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua


Njia zingine za kupata mimba ya mapacha


Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wanaotungisha mimba kwa kusaidiwa, yaani mtungisho kufanyikia kwenye chupa kisha kupandikizwa, wana hatari ya kupata mimba ya mapacha au zaidi kwa asilimia inayofikia 40.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

7 Oktoba 2021 04:58:02

Rejea za mada hii:

1. de Mouzon J, et al. Assisted reproductive technology in Europe, 2007: results generated from European registers by ESHRE. Human Reproduction. 2012;27(4):954–966

2. Society for Assisted Reproductive Technology. Assisted reproductive technology in the United States: 2001 results generated from the American Society for Reproductive Medicine/Society for Assisted Reproductive Technology registry. Fertility and Sterility. 2001;87:1253–1266

3. Moise J, et al. The outcome of twin pregnancies after IVF. Human Reproduction. 1998;13(6):1702–1705

4. Spellacy WN, et al. A case-control study of 1253 twin pregnancies from a 1982–1987 perinatal data base. Obstetrics and Gynecology. 1990;75(2):168–171

5. Ozturk O, et al. Multiple pregnancy in assisted reproduction techniques. In: Vayena E, Rowe PJ, Griffin PD, editors. Current Practices and Controversies in Assisted Reproduction. Geneva, Switzerland: WHO; 2002. pp. 220–234

6. Dhont M, et al. Perinatal outcome of pregnancies after assisted reproduction: A case-control study. American Journal of Obstetrics and Gynecology. 1999;181(3):688–695

7. FIGO Committee for the Ethical Aspects of Human Reproduction and Women's Health. Ethical guidelines in the prevention of iatrogenic multiple pregnancy. European Journal of Obstetrics & Gynecology and Reproductive Biology. 2001;96:209–210

8. Thorpe K, et al. Comparison of prevalence of depression in mothers of twins and mothers of singletons. British Medical Journal. 1991;302(6781):875–878

9. Kinzler WL, et al. Medical and economic effects of twin gestations. Journal of the Society for Gynecologic Investigation. 2000;7(6):321–327

10. ASRM Guidelines on number of embryos transferred. A Practice Committee Report. pp. 1-2, November 1999

11. Ida Lilywaty Md Latar, et al. The Desire for Multiple Pregnancy among Patients with Infertility and Their Partners. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4334053/. Imechukuliwa 27.07.2021

12. John Collins, et al. Global epidemiology of multiple birth. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/18598609/. Imechukuliwa 27.07.2021

13. ART success rates. cdc.gov/art/reports/index.html. Imechukuliwa 27.06.2021

14. Assisted reproductive technology. nichd.nih.gov/health/topics/infertility/conditioninfo/Pages/art.aspx. Imechukuliwa 27.06.2021

15. Being pregnant with twins, triplets, and other multiples. marchofdimes.org/pregnancy/multiples-twins-triplets-and-beyond.aspx. Imechukuliwa 27.06.2021

16. Clomiphene. mayoclinic.org/drugs-supplements/clomiphene-oral-route/description/drg-20063072

17. Derom C,et al. . High frequency of iatrogenic monozygotic twins with administration of clomiphene citrate and a change in chorionicity. Fertility and Sterility, 85(3), 755-757
sciencedirect.com/science/article/pii/S001502820503949X. Imechukuliwa 27.06.2021

18. Fertility drugs and the risk of multiple births. asrm.org/FACTSHEET_Fertility_Drugs_And_The_Risk_Of_Multiple_Births/. Imechukuliwa 27.06.2021

19. Having twins. acog.org/-/media/For-Patients/faq092.pdf?dmc=1&ts=20150917T1925392575. Imechukuliwa 27.06.2021

20. Martin J, et al. Three decades of twin births in the United States, 1980-2009. cdc.gov/nchs/data/databriefs/db80.htm. Imechukuliwa 27.06.2021

21. Multiple pregnancy and birth: twins, triplets, and high-order multiples. asrm.org/BOOKLET_Multiple_Pregnancy_and_Birth/. Imechukuliwa 27.06.2021

22. North Shore-Long Island Jewish Health System. (2006, May 20). Study finds that a woman’s chance of having twins can be modified by diet. eurekalert.org/pub_releases/2006-05/nsij-sft051606.php. Imechukuliwa 27.06.2021

23. Pregnant with twins. nhs.uk/conditions/pregnancy-and-baby/pages/what-causes-twins.aspx#close. Imechukuliwa 27.06.2021

24. Side effects of injectable fertility drugs (gonadotropins). asrm.org/FACTSHEET_Side_effects_of_injectable_fertility_drugs_gonadotropins/. Imechukuliwa 27.06.2021

25. American Society for Reproductive Medicine. Multiple Pregnancy and Birth: Twins, Triplets, and High Order Multiples (booklet). Imechukuliwa 27.06.2021

26. McDonald S, et al. Perinatal outcomes of in vitro fertilization twins: A systematic review and meta-analyses. Am J Obstet Gynecol. 2005;193(1):141-152. doi:10.1016/j.ajog.2004.11.064

27. U.S. Food and Drug Administration. CLOMID® (clomiphene citrate tablets USP). Sanofi-Aventis U.S. LLC. Imechukuliwa 27.06.2021

28. Glinianaia SV, et al. Prevalence, antenatal management and perinatal outcome of monochorionic monoamniotic twin pregnancy: A collaborative multicenter study in England, 2000-2013. Ultrasound Obstet Gynecol. 2019;53(2):184-192. doi:10.1002/uog.19114

bottom of page