top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, M.D

Mhariri:

Dkt. Adolf S, M.D

Jumapili, 23 Julai 2023

Unapima mara ngapi VVU baada ya kuanza PEP?

Unapima mara ngapi VVU baada ya kuanza PEP?

Mara baada ya kuanza PEP utapangiwa ratiba ya kurudia kipimo cha HIV miezi mitatu tangu siku ya kuwa kwenye kwenye kihatarishi. Haishauriwi kupima VVU au kuonana na mtaalamu ndani ya siku 28 toka umejihatarishi, hata hivyo unashauriwa kutafuta msaada haraka endapo utapata maudhi yoyote ya dawa yanayoweza kuingilia utumiaji wa dawa za PEP.Kila unapohudhuria kliniki utaendelea kusisitizwa umuhimu wa kutumia na kumaliza dozi ya PEP kikamilifu na kupunguza hatari ya kujianika kwenye kihatarishi kingine wakati unaendelea na dozi.


Endapo itathibitika kuwa chanzo cha maambukizi hakina maambukizi ya VVU, utashauriwa kusitisha dawa.


Je ni mara ngapi utapaswa kupima VVU baada ya kuanza PEP?

Watu wote waliojianika kwenye VVU wanashauriwa kupima maambukizi ya VVU miezi 3 na 6 baada ya kujihatarisha. Vipimo zaidi baada ya muda huu vitafanyika endapo kuna kihatarishi endelevu, una ujauzito na upo kwenye maeneo yenye hali kubwa ya maambukizi ya VVU au kuwa na majibu tata.


Makundi yanayayopaswa kupima kila baada ya miezi 3

Makundi aina fulani tu ya watu walio kwenye maeneo yenye maambukizi ya hali ya juu ya VVU na kuwa na kihatarishi cha kupata maabukizi wanahitaji kupima VVU kila baada ya miezi mitatu. Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linapendekeza makundi yafuatayo kurudia vipimo;

  • Watu wote walio kwenye maeneo ya hatari kubwa ya maambukizi ya VVU

  • Watu wenye vihatarishi endelevu vya kupata VVU

  • Watu walio kwneye kundi maalumu ambalo ni wafungwa, wanaume wanaofanya ngono na wanaume, wanaotumia dawa za kulevya kwa kujidunga sindano, wauzaji mwili kwa ngono na waliobadilisha jinsia.

  • Vijana wadogo waishio Kusini mwa Afrika sehemu yenye hatari kubwa ya maambukizi

  • Watu wanaoishi na wenza wenye VVU


Kipimo cha VVU kinaweza kurudiwa pia endapo;
  • Una dalili za au kupata matibau ya magonjwa ya zinaa au virusi vya homa ya ini

  • Umehisiwa kuwa na TB kwa dalili au kutambulika kwa Vipimo

  • Una dalili au ishara zinazoashiria maambukizi ya VVU

  • Umejihatarisha hivi karibuni kwenye maambukizi ya VVU


Hitimisho

Kupima mara kwa mara maanake ambayo ni kila baada ya miezi 3 hadi 6 kunaweza kupendekezwa kwa watu walio kwenye hatari ya maambukizi. Watu wasio na kihatarishi endelevu hawana ulazima wa kupima mara kwa mara kuepuka upotevu wa rasilimali. Endapo kihatarishi ni endelevu njia za kujikinga zinashauriwa kutumika kama vile matumizi ya PrEP na Kondomu.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 09:19:12

Rejea za mada hii:

WHO. CONSOLIDATED GUIDELINES ON HIV TESTING SERVICES FOR A CHANGING EPIDEMIC @2019

bottom of page