Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Helen L, M.D
Jumapili, 31 Januari 2021
Usifanye ‘dieting’ kupunguza uzito, uepuke ongezeko la uzito mara mbili zaidi ya uliopoteza
Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa, asilimia 80 hadi 90 ya watu wanaofanya ‘dieting’, baada ya kupungua na kufikia malengo ya uzito wanaoutaka na kuacha, miili yao hupata ongezeka la uzito mara mbili ya ule ulioupotea kwa kufanya ‘dieting’. Kula vema kila siku kama mbadala wa kufanya ‘dieting’
Dieting ni nini?
‘Dieting’ ni kitendo cha kuzingatia utumiaji wa chakula na vinywaji kwa lengo la kupunguza, kuongeza au kubaki na uzito ulionao kama njia ya kujikinga au kutibu magonjwa kama shinikizo la juu la damu, kisukari na obeziti.
Watu wengi duniani wamekuwa wakitumia njia ya ‘dieting’ ili kupunguza uzito. Njia hii ya ‘dieting’ ni njia nzuri ya kupunguza uzito kwa muda mfupi lakini kwa bahati mbaya si njia inayoshauriwa kiafya. Matumizi ya njia hii hufanya mwili ujipe adhabu ya kuongezeka uzito mara dufu zaidi ya ule wa awali mara baada ya kuacha kufanya ‘dieting’. Unashauriwa kutumia njia za kiafya kupunguza uzito badala ya kufanya ‘dieting’.
Sababu za uzito kujirudia mara dufu baada ya kuacha kufanya ‘dieting’
Wanasayansi wamefanya uchunguzi wa mwili wa binadamu kwa miaka kadhaa na kugundua kuwa, homoni zinazotolewa kwenye utumbo, kongosho na kutoka kwenye mafuta huchangia kwa kiasi kikubwa kurekebisha uzito, hisia za njaa pamoja na matumizi ya nishati mwilini. Wakati unajizuia kula vyakula aina fulani ili kupunguza uzito, mabadiliko ya homoni mwilini mwako hutokea, yanayofanya ubongo utume taarifa ya kukabiliana na mabadiliko hayo. Kwa mfano, endapo kiwango cha mafuta kimepungua mwilini, kiwango cha homoni leptin kinachouambia ubongo kwamba umeshiba hupungua, na kiwango cha homoni za kuongeza njaa kama ghrelin huongezeka na kusabisha upate njaa na ule sana. Kujinyima kwa muda mfupi kula vyakula aina fulani kwa lengo la kupunguza uzito, husababisha mabadiliko ya muda mfupi ambayo huamsha mwili wako kurejesha uzito wa awali kwa kuongeza homoni zinazoleta njaa na kusababisha upende kula zaidi, na hivyo kuongezeka uzito mara dufu.
Njia nzuri za kuwa na uzito wa kiafya
Kula matunda na mboga za majani kwa wingi
Acha kula vyakula na vinywaji vyenye sukari kama soda, keki na pipi
Tumia mafuta ya kiafya kutoka yanayotokana na mimea kama, mzeituni, karanga, ufuta, alizeti n.k yatakayokufanya ujihisi umeshiba na kupunguza unene
Fanya mazoezi ya kutoa jasho na kufanya misuli ifanye kazi mfano, tembea mwendao wa dakika 30 kwa siku, lima, palilia bustani, endesha baiskeli n.k
Fanya mazoezi ya misuli ili kufanya misuli yako ifanye kazi na kutumia sukari iliyo kwenye damu
Kula chakula ulichokipika mwenyewe badala ya kula mgahawani au hotelini ili kujiepusha na viungo vinavyoongeza uzito pia ufurahie ladha ya chakula chako mwenyewe.
Pata kifungua kinywa chenye protini kwa wingi mfano mayai, maziwa mgando, nyama ya samaki, juisi yenye maziwa mtindi n.k badala ya wanga
Usitumie vinywaji wa kuongeza nguvu, kama vinywaji vya wanamichezo, ‘energy drink’ n.k, badala yake tumia maji
Kunywa maji ya kutosha kila siku, kunywa maji ya uvuguvugu dakila 30 kabla ya kula mlo mzito
Epuka kula kila kinachokuja mbele yako, kula kwa ratiba uliyojipangia
Usitumie mazao ya vyakula vilivyokobolewa kama mahindi, n.k
Usitumie vyakula vya kupunguza uzito
Kuwa na timu ya marafiki wenye malengo ya kufanya mazoezi na kula vema
Unapokuwa na mawazo au msongo, jipe muda wa kufanya vitu/mambo unavyopenda kufanya ili kuepuka mawazo mengi yanayoweza kupelekea kula sana na kuongezeka uzito
Penda kutumia vyakula asilia kama mbadala wa vyakula vya kusindikwa
Penda kujifunza kuhusu mambo ya kiafya na njia salama za kuwa na uzito unaotakiwa kiafya
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:41:55
Rejea za mada hii:
1.JS Vander Wal, A Gupta, et al. Egg breakfast enhances weight loss. https://www.nature.com/articles/ijo2008130. Imechukuliwa 30.01.2021
2.G Harvey Anderson, et al. Effect of glycemic carbohydrates on short-term satiety and food intake. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/12828188. Imechukuliwa 30.01.2021
3.Michail Mantzios. Mindfulness, Eating Behaviours, and Obesity: A Review and Reflection on Current Findings. https://link.springer.com/article/10.1007%2Fs13679-014-0131-x. Imechukuliwa 30.01.2021
4.Tammy Chang et al. Inadequate Hydration, BMI, and Obesity Among US Adults: NHANES 2009–2012. http://www.annfammed.org/content/14/4/320. Imechukuliwa 30.01.2021
5.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/20226994. Imechukuliwa 30.01.2021
6.Catherine M. Champagne, et al. Dietary intakes associated with successful weight loss and maintenance during the Weight Loss Maintenance Trial. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3225890/. Imechukuliwa 30.01.2021
7.Michelle J Clark, et al. The effect of fiber on satiety and food intake: a systematic review. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/23885994. Imechukuliwa 30.01.2021
8.G A Bray, et al. Calorie-sweetened beverages and fructose: what have we learned 10 years later. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/23625798. Imechukuliwa 30.01.2021
9.George A Bray, et al. Dietary sugar and body weight: have we reached a crisis in the epidemic of obesity and diabetes?: health be damned! Pour on the sugar. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/24652725. Imechukuliwa 30.01.2021
10.J Bond Brill, et al. Dose-response effect of walking exercise on weight loss. How much is enough?. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/12439651. Imechukuliwa 30.01.2021
11.Arpita Tiwari, MHS, et al. Cooking at Home: A Strategy to Comply With U.S. Dietary Guidelines at No Extra Cost. http://www.ajpmonline.org/article/S0749-3797(17)30023-5/fulltext. Imechukuliwa 30.01.2021
12.Julia A Wolfson, et al. Is cooking at home associated with better diet quality or weight-loss intention?. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/25399031. Imechukuliwa 30.01.2021
13.Dr. Ramon Estruch, MD, et al. Retracted: Effect of a high-fat Mediterranean diet on bodyweight and waist circumference: a prespecified secondary outcomes analysis of the PREDIMED randomised controlled trial. http://www.thelancet.com/journals/landia/article/PIIS2213-8587(16)30085-7/abstract. Imechukuliwa 30.01.2021
14.Erik Scott Blomain, et al. Mechanisms of Weight Regain following Weight Loss. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3901982/. Imechukuliwa 30.01.2021
15.Kevin D. Hall , et al. Maintenance of lost weight and long-term management of obesity. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5764193/. Imechukuliwa 30.01.2021