Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Sospeter M, MD
Jumapili, 25 Julai 2021
Utumiaji wa testosterone
Testosterone ni homoni ya kiume jamii ya steroidi inayongeza hamu ya ngono, uzito wa mifupa, damu, misuli na hali ya moyo. Unashauriwa kutotumia testosterone wakati usio sahihi.
Kiwango cha kawaida cha testosterone ni ngapi?
Kwa kawaida, kiwango cha kawaida cha homoni testosterone kwenye damu kwa wanaume ni kati ya nanogramu 300 hadi 1,000 kwa desilita moja ya damu. Wanawake pia huwa na kiwango kidogo sana cha homoni hii.
Utambuzi na dalili za upungufu wa homon testosterone
Kwa kawaida kiwango cha homon testosterone hupungua kwenye damu kwa wanaume kuanzia umri wa miaka 30 hadi 40. Kupungua kwa haraka au kabla ya umri huu husababisha dalili za upungufu ambazo ni;
Kushindwa simamisha uume au kutosimama kwa muda mrefu
kupungua hamu ya mapenzi
Kupungua kwa kiwango cha manii kwenye shahawa
Sonona na wasiwasi
Kuongezeka uzito
Kuwa na vipindi vya kutokwa na jasho usoni
Kuimba kwa chuchu
Kubadilika maumbile ya korodani na uume
Namna gani upungufu wa cha testosterone kwenye damu hutambuliwa?
Kiwango cha testosterone hutambuliwa kwa kufanya kipimo cha kinachopima kiwango cha homon hii kwenye damu. Baadhi ya watu huta hivyo hujipima kwa dalili, hii si sahihi kwa sababu kiwango hiki kinaweza kupungua jinsi umri unavyoenda na njia pekee inabadi kufanya kipimo cha kiwango cha homoni hii kwenye damu.
Faida za sindano ya testosterone na wakati wa kuchoma?
Kutumia sindano ya testosterone huongeza;
Hamu ya ngono
Nguvu za mwili
Muda wa uume kusimama
Hali ya mtu
Kiwango cha manii kwenye shahawa
Ukubwa wa misuli na kupunguza mafuta maeneo ya tumbo
Wakati gani unahitajikuchoma sindano ya testosterone?
Kama kiwango cha homoni testosterone kipo chini zaidi ya kawaida,na kuwa na dalili za upugnufu wa homon hii, utashauriwa na daktari kuchoma dawa ya testosterone ili kurejesha kiwango katika hali ya kawaida. Mtumiaji wa dawa hii atapaswa kuchoma kila baada ya wiki nne au kwa jinsi atakavyoshauriwa kulingana na tatizo lake.
Maudhi, madhara na tahadhari ya kuchoma sindano ya testosterone
Je upungufu wa testosterone husababisha kiwango cha manii kuwa kidogo kwenye shahawa?
Jibu la swali hili ni ndio na hapana
Mara nyingi watu wenye kiwango kidogo cha manii kwenye shahawa au wasio na manii kabisa kwenye shahawa huwa na kiwango cha kawaida cha testosterone kwenye damu. Tafiti zinaonyesha kuchoma sindano ya testosterone kunaweza ongeza uzalishaji kwa watu wenye kiwango cha chini na kupunguza uzazlishaji wa manii kwa wanaume wenye kiwango cha kawaida. Matumizi ya testosterone kwa wingi pia hupunfuza uzalishaji wa manii.
Maudhi ya kuchoma testosterone
Kuongezeka kwa chunusi
Kutuwama kwa maji mwilini
Kukojoa sana
Kukua kwa titi
Kupungua korodani
Kupungua kwa manii
Kuwa na tabia haribifu
Kukosa pumzi wakati wa kulala kwa wazee
Madhara ya kutumia testosterone
Ingawa kuchoma testosterone huwasaidia wanaume wenye upungufu wa homoni hii, baadhi ya wanaume haswa wenye kiwango cha kawaida huweza kupata;
Magonjwa ya moyo kama mshituko wa moyo
Kuganda kwa damu
Matatizo ya ini
Kiharusi
Dalili kali za saratani ya tezi dume au kuongezeka haraka kwa kwa tezi dume iliyokuwa
Watu gani hawapaswi kuchoma testosterone?
Watu wenye matatizo yafuatayo hawapaswi kutumia testosterone
Wenye saratani ya tezi dume
Wenye saratani ya titi
Tahadhari kwa watumiaji wa testosterone
Tahadhari inapaswa kuchukuliwa kwa wagonjwa wenye
Matatizo ya moyo
Damu nyingi
Kukosa pumzi wakati wa kulala
Njia asili za kuongeza kiwango cha testosterone kwenye damu
Kuna vyakula ambavyo vinaweza kuongeza homon testosterone kwenye damu, vyakula hivyo msingi wake ni kuwa na vitamin D na madini ya zinki kwa wingi ambayo huhusiana na uzalishaji wa homoni hii pamoja aa manii. Utahitaji kuwa mtumiaji wa muda mrefu ili upate faida zake. Miongoni mwa vyakula hivyo ni;
Kiini cha yai
Samaki jamii ya tuna
Kaa
Uduvi
Maziwa yaliyopunguzwa mafuta na kutiwa vitamin D
Unga uliotiwa virutubisho
Maharagwe
Karanga
Mbegu za boga
Njia nyingine asili za kuongeza kiwango cho homoni testosterone ni;
Kufanya mazoezi yenye mpangilio maalumu
Kulala muda unaokubalika kiafya
Kupunguza matumizi ya vyakula vyenye sukari kwa wingi
Kupunguza mafuta mwilini kwa kupunguza uzito
Kupata kiwango cha madini nyongeza ya zinki
Kula mlo kamili unaokubalika kiafya
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
7 Oktoba 2021 05:04:48
Rejea za mada hii:
1. Bassil N, et alThe benefits and risks of testosterone replacement therapy: a review. Therapeutics and Clinical Risk Management, 5, 427-448
ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2701485/. Imechukuliwa 23.07.2021
2. Fredman L, et al. Testosterone (T) nasal gel (Natestoâ„¢) improves erectile dysfunction and mood in hypogonadal men. Canadian Journal of Diabetes, 40(5), S35-S36. canadianjournalofdiabetes.com/article/S1499-2671(16)30386-0/fulltext?rss=yes. Imechukuliwa 23.07.2021
3. Gallenberg, et al. Does testosterone therapy help increase sex drive in women? What are the pros and cons?. mayoclinic.org/diseases-conditions/menopause/expert-answers/testosterone-therapy/faq-20057935. Imechukuliwa 23.07.2021
4. Lang T. F. The bone-muscle relationship in men and women. Journal of Osteoporosis, 2011. hindawi.com/journals/jos/2011/702735/. Imechukuliwa 23.07.2021
5. Mayo Clinic. Testosterone therapy: Potential benefits and risks as you age. mayoclinic.org/healthy-lifestyle/sexual-health/in-depth/testosterone-therapy/art-20045728. Imechukuliwa 23.07.2021
6. Snyder, P. J, et al. Ellenberg, S. S. (2016, February 16). Effect of testosterone treatment in older men. The New England Journal of Medicine, 374, 611-624. nejm.org/doi/full/10.1056/NEJMoa1506119 - t=article. Imechukuliwa 23.07.2021
7. Study questions benefits of testosterone replacement for low T. sciencedaily.com/releases/2016/09/160921145344.htm. Imechukuliwa 23.07.2021
8. Study of 83,000 veterans find cardiovascular benefits to testosterone replacement. research.va.gov/currents/0815-5.cfm. Imechukuliwa 23.07.2021
9. Turner, et al. Testosterone increases bone mineral density in female-to-male transsexuals: a case series of 15 subjects. Clinical Endocrinology (Oxf), 61(5), 560-566. ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3098904/. Imechukuliwa 23.07.2021
10. Morris P.D, et al. Testosterone and cardiovascular disease in men. Asian Journal Andrology, (3):428-35. ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/22522504/. Imechukuliwa 23.07.2021
11. Chang, C. S, et al. Correlation between serum testosterone level and concentrations of copper and zinc in hair tissue. Biological Trace Element Research, 144(1-3), 264-271. ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/21671089. Imechukuliwa 23.07.2021
12. Corona, G., et al. Body weight loss reverts obesity-associated hypogonadotropic hypogonadism: a systematic review and meta-analysis. European Journal of Endocrinology, 168(6), 829-843. ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/23482592. Imechukuliwa 23.07.2021
13. Grossmann, M. Testosterone and glucose metabolism in men: current concepts and controversies. Journal of Endocrinology, 220(3), R37-55. ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/24353306. Imechukuliwa 23.07.2021
14. How much sleep do we really need?. sleepfoundation.org/article/how-sleep-works/how-much-sleep-do-we-really-need. Imechukuliwa 23.07.2021
15. Leproult R, et al. Effect of 1 week of sleep restriction on testosterone levels in young healthy men. Journal of the American Medical Association, 305(21), 2173-2174. jama.jamanetwork.com/article.aspx?articleid=1029127. Imechukuliwa 23.07.2021