top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

Alhamisi, 9 Septemba 2021

Uwezo tambuzi na usahihi wa vipimo vya VVU

Uwezo tambuzi na usahihi wa vipimo vya VVU

Kutokana na uwezo tambuzi na usahihi wa chini ya asilimia 100 wa vipimo vingi vya VVU, majibu chanya yataaminika kama zaidi ya aina moja ya kipimo itatumika.


Aina ya vipimo vya VVU


Kuna aina nyingi za vipimo vya haraka vya VVU vinavyopatikana duniani. Aina hizo hutofautiana uwezo tambuzi na usahihi kwenye kutambua uwepo wa VVU mwilini. Mfano wa vipimo hivyo ni;


  • First Response HIV Card Test 1–2.0.

  • Uni-Gold HIV

  • HIV 1/2 STAT-PAK

  • Vikia HIV 1/2

  • Determine HIV-1/2

  • Genie Fast HIV ½

  • INSTI HIV-1/HIV-2 Antibody Test

  • SD Bioline HIV 1/2 3.0


Mifano ya namna vipimo vinavyoweza kutoa majibu yasiyo sahihi


Mfano wa kwanza

Ukipima maambukizi ya VVU kwa watu 10,000 kwa kutumia vipimo aina tatu tofauti kwenye eneo endapo hali ya maambukizi ya VVU katika eneo hilo lenye hali ya maambukizi ya asilimia 1, pasipo kurudia kipimo, watu 9 wasio na VVU wataanzishiwa dawa na kutumia kwa maisha yao yote hali kwamba hawana VVU


Mfano wa pili

Ukipima maambukizi ya VVU kwa watu 10,000 kwa kutumia vipimo aina tatu tofauti kwenye eneo endapo hali ya maambukizi ya VVU katika eneo hilo lenye hali ya maambukizi ya asilimia 19, pasipo kurudia kipimo, watu 39 wasio na maambukizi ya VVU wataanzishiwa dawa na kutumia kwa maisha yao yote hali kwamba hawana VVU.


Uwezo tambuzi wa vipimo vya haraka vya VVU


Uwezo tambuzi wa kipimo ni uwezo wa kipimo kutoa majibu chanya kwa mwenye maambukizi ya VVU unaopimwa kwa asilimia.


Baadhi ya vipimo na uwezo tambuzi wake vimeorodheshwa hapa chini


Uwezo tambuzi wa 98.8%

  • First Response HIV Card Test 1–2.0.


Uwezo tambuzi wa 99.5%

  • Uni-Gold HIV

  • HIV 1/2 STAT-PAK

  • Vikia HIV 1/2


Uwezo tambuzi wa 100%

  • Determine HIV-1/2

  • Genie Fast HIV 1/2

  • INSTI HIV-1/HIV-2 Antibody Test

  • SD Bioline HIV 1/2 3.0


Usahihi/Umahususi wa vipimo vya VVU


Usahihi wa kipimo ni uwezo wa kipimo kutoa majibu hasi kwa magonjwa asiye na maambukizi ya VVU na hupimwa kwa asilimia. Kipimo chenye asilimia kidogo ya usahihi hutoa majibu chanya isiyo sahihi kwa wingi.


Mafano wa vipimo na usahihi wake kutoa majibu hasi ya VVU


Usahihi kati ya 90% na 95%

  • First Response HIV Card Test 1–2.0

  • INSTI HIV-1/HIV-2 Antibody Test

  • Determine HIV-1/2

  • Genie Fast HIV 1/2


Usahihi kati ya 97% na 98%

  • Vikia HIV 1/2

  • SD Bioline HIV 1/2 3.0

  • Uni-Gold HIV


Usahihi wa 99.7%

  • HIV 1/2 STAT-PAK.


Mambo yanayopunguza uwezo tambuzi na usahihi wa vipimo vya VVU


Kuna mambo mbalimbali yaliyoonekana kwenye tafiti kudhuru uwezo tambuzi na usahihi wa majibu ya vipimo vya haraka vya VVU ambayo ni;


  • Kuwa mwanaume (INSTI, Vikia na Genie Fast test)

  • Kuwa na magonjwa mengine mbali na VVU (Kipimo cha Determine )

  • Eneo unaloishi-nchi (kipimo cha INSTI, SD Bioline na First Response test)


Namna ya kuongeza uwezo wa utambuzi na kupata majibu sahihi ya VVU


Ili kuongeza uwezo wa utambuzi na kupata majibu sahihi, unapaswa kutumia zaidi ya kipimo kimoja yaani angalau vipimo vitatu tofauti. Mfano nchi nyingi za Afrika zimeshauriwa na WHO kutumia angalau SD Bioline HIV 1/2 3.0 na Uni-Gold HIV1/2 Baada ya kutumia SD Bioline HIV 1/2 3.0 na majibu kuwa chanya, cha Uni-Gold HIV1/2 hutumika mara nyingi, na majibu ya kipimo yakiwa chanya, basi mgonjwa husemekana kuwa na maambukizi. Hata hivyo kabla ya mteja kuanzishiwa dawa za ARV, wiki kadhaa baada ya kugundulika na maambukizi, anapswa rudia kipimo upya yaani kipimo cha SD Bioline HIV 1/2 3.0 na Uni-Gold HIV1/2.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

7 Oktoba 2021 05:05:58

Rejea za mada hii:

Kosack CS et al. Towards more accurate HIV testing in sub-Saharan Africa: a multi-site evaluation of HIV RDTs and risk factors for false positives. Journal of the International AIDS Society 20:21345, 2017. http://www.jiasociety.org/index.php/jias/article/view/21345/html. Imechukuliwa 09/09/2021

Eaton JW et al. The cost of not re-testing: HIV misdiagnosis in the ART ‘test-and-offer’ era. Clinical Infectious Diseases, online ahead of print, 2017. https://academic.oup.com/cid/article/3751368/The-cost-of-not-re-testing-HIV-misdiagnosis-in-the. Imechukuliwa 09/09/2021

Pascale Chaille, et al. Evaluation of four rapid tests for diagnosis and differentiation of HIV-1 and HIV-2 infections in Guinea-Conakry, West Africa. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/20708123/. Imechukuliwa 09/09/2021

AIDS map. Avoiding false positives: rapid HIV tests vary in their accuracy, so need to be used in combination. https://www.aidsmap.com/news/may-2017/avoiding-false-positives-rapid-hiv-tests-vary-their-accuracy-so-need-be-used. Imechukuliwa 09/09/2021

WHO Prequalification of In Vitro Diagnostics Programme. PUBLIC REPORT Product: INNO-LIA HIV I/II Score Number: PQDx 0203-073-00. https://extranet.who.int/pqweb/sites/default/files/PQDx_0203-073-00_InnoLiaHIV_Score_v2.pdf. Imechukuliwa 09/09/2021

bottom of page