top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

Dkt. Helen L, M.D

17 Aprili 2025, 12:48:47

Uzito wa mtoto katika umri wa miaka miwili ya kwanza

Uzito wa mtoto katika umri wa miaka miwili ya kwanza

Mtoto huongezeka uzito wake mara mbili kabla ya kufikisha miezi sita, mara tatu anapofikisha mwaka mmoja, na mara nne (quadruple birth weight) anapofikisha miaka miwili. Ongezeko hili ni makadilio ya ukuaji wa kawaida yanayotegemea lishe, afya, na mazingira, na hutumika kutambua mapema matatizo ya ukuaji. Kufuatilia mwendo wa uzito kunasaidia kuhakikisha mtoto anapata virutubisho vya kutosha kwa maendeleo yake.


Uzito mara mbili

Katika miezi 4–6 ya kwanza, mtoto huongezeka uzito mara mbili ya uzito aliouzaliwa nao. Kati ya kipindi hiki, ongezeko la uzito hupunguza kidogo kutoka kiwango cha kuzaliwa hadi kuhama kwenye vyakula vingine.


Uzito Maratatu

Kati ya miezi 6 na 12, mtoto huongeza uzito hadi mara tatu ya uzito alizaliwa nao. Ongezeko la uzito hupungua kidogo kulinganisha na kipindi cha awali, likiwa takriban gramu 50–75 kwa wiki.


Uzito mara nne

Kati ya miezi 12 na 24, mtoto hhuongezeka uzito mara nne ya uzito alizaliwa nao. Ingawa ukuaji wa uzito hupungua kidogo ukilinganisha na kipindi cha kwanza, bado ni muhimu kwa ukuaji wa misuli na seli nyingine za mwili.


Maelezo zaidi na mipangilio ya kiafya


Vigezo vya WHO na CDC

Vigezo vya WHO vinatoa chati za ukuaji kwa umri wa kuzaliwa hadi miaka mitano. CDC hutumia chati hizi pamoja na chati za kitaifa ili kufuatilia ukuaji wa watoto. Watoto wanaoonyesha tofauti kubwa kuliko viwango hivi wanashauriwa kupimwa na mtaalamu wa afya kwa uchunguzi wa kina.


Michango ya lishe na ushauri
  • Maziwa ya mama au mbadala bora: Yanapendekezwa kiasi kikubwa hadi miezi 6, kisha kuanzisha vyakula vya nyongeza polepole.

  • Vyakula vyenye protini: Maharage, samaki, dagaa, mayai na nyama laini husaidia ukuaji wa misuli na tishu.

  • Wanga na mafuta mazuri: Viazi, wali, ndizi, chapati, mafuta ya alizeti na siagi ya karanga huongeza kalori na nguvu.

  • Mboga na matunda: Parachichi, papai, embe, mchicha na kisamvu vinatoa vitamini na madini muhimu kwa kinga na ukuaji wa seli.


Ufuatiliaji na ulinganisho
  1. Pima uzito mara kwa mara: Kila mwezi hadi miezi 6, kisha kila 2–3 miezi hadi miaka 2, na kila 6 miezi hadi miaka 5.

  2. Tumia chati za ukuaji rasmi: Rekodi uzito na umri kwenye chati ya WHO/CDC ili kuona mwenendo.

  3. Tafuta msaada wa mtaalamu: Endapo uzito wa mtoto uko chini sana, wasiliana na daktari au mtaalamu wa lishe.


Hitimisho

Ongezeko la uzito mara mbili kwa miezi 6, mara tatu kwa mwaka mmoja, na mara nne kwa miaka 2 ni makadilio muhimu ya ukuaji wa kawaida. Kufuatilia viwango hivi pamoja na lishe bora kunaweka msingi wa afya njema ya mtoto wako. Kumbuka, kila mtoto ni wa kipekee—zingatia ushauri wa kiafya na endelea kumpa msaada unaofaa.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeandikwa:

19 Januari 2021, 06:01:02

Rejea za mada hii:

1. World Health Organization. Child growth standards: length/height-for-age, weight-for-age, weight-for-length, and body mass index-for-age. Geneva: World Health Organization; 2006. Available from: https://www.who.int/childgrowth/standards/en/

2. Centers for Disease Control and Prevention (CDC). Growth charts. 2020. Available from: https://www.cdc.gov/growthcharts/

3. American Academy of Pediatrics. Pediatric nutrition. 7th ed. Elk Grove Village, IL: American Academy of Pediatrics; 2014.

4. Dewey K, Brown K. Update on the status of research into the role of complementary feeding in the prevention of childhood malnutrition. Am J Clin Nutr. 2003;78(4):880-7. doi: 10.1093/ajcn/78.4.880.

5. Lutter C, Daelmans B, Dewey K, et al. Global strategy for infant and young child feeding. World Health Organization. 2003. Available from: https://www.who.int/nutrition/topics/infantfeeding/en/

6. Ruel MT, Menon P, Loewenson R. A methodology for evaluating the effectiveness of complementary feeding programs. J Nutr. 2001;131(4):1204S-1210S.

7. Thurnham DI, Northrop-Clewes CA. Micronutrients in the human diet and nutrition. Asia Pacific Journal of Clinical Nutrition. 2003;12(S1):S3-S5.

8. Guo SS, Chumlea WC, Roche AF, Kuczmarski RJ, Flegal KM. Influence of age on the stature-weight indices. Am J Clin Nutr. 1994;59(1):69-75.

bottom of page