Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Sospeter M, MD
Ijumaa, 6 Agosti 2021
Viungo vya chakula kwa mjamzito
Viungo vingi vya chakula ni salama kwa mama mjamzito kama vitatumika kwa kiasi, hata hivyo baadhi yake pia huweza anzisha uchungu, kutoa mimba na madhaifu kwa mtoto. Baadhi ya viungo vya kuepuka au kutumiwa kwa kiasi kidogo sana ni vitunguu swaumu, mbegu za ufuta, uwatu na mdalasini.
Je unapaswa kutumia viungo vingi kupita kiasi hata kama ni vya umuhimu?
Hapana!
Viungo vyovyote vile vyenye virutubisho muhimu kwa afya ya ujauzito ni vizuri kutumika kwa mjamaizto, hata hivyo unapaswa kuwa makini na baadhi ya viungo vinavyofahamika kusababisha madhara kwa mjamzito.
Ikumbukwe pia, viungo hutumika katika tiba asilia kama dawa, hivyo matumizi kwa kiasi kikubwa ya viungo huweza kusababisha madhara.
Orodha ya viungo muhimu na faida zake
Pipilipi manga
Huwa na madini mengi ya chromium, yenye umuhimu sana kwa mjamzito. Upungufu wa madini haya huongeza kiwango cha lehemu na sukari kwenye damu kinachoongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kisukari. Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wenye kisukari cha ujauzito kama watapata chakula chenye madini chromium, huwasaidia kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu. Hata hivyo baada ya kujifungua, matumizi ya uji wenye pilipili manga huchochea uzalishaji wa maziwa mengi.
Pilipili nyeupe
Pilipili nyeupe huwa na uwezo wa kuzuia hali ya kupata choo kigumu inayotokea sana kwa wajawazito.
Tangawizi
Kwa wanawake wenye kichefuchefu na kutapika, tangawizi ni tiba asili ya kupunguza kichefuchefu na kutapika au homa ya ujauzito inayotokea sana wakati wa asubuhi. Matumizi ya gramu moja ya tangawizi kwa siku kwa siku nne mfululizo hupunguza hali nah ii imethibitishwa na tafiti mbalimbali.
Iliki
Matumizi ya iliki husaidia kuzuia damu kuganda, hali inayotokea sana kutokana na ujauzito na kufanya kuwa moja ya kiungo muhimu kutumiwa kwenye chakula wakati wa ujauzito.
Jira
Kitiba asilia, jira hutumika kama dawa ya kupunguza michomo kinga na kuzuia gesi tumboni wakati wa ujauzito.
Manjano
Licha ya kuwa na uwezo wa kupunguza maumivu na kuimarisha afya ya ngozi, manjano huwa na virutubisho vinavyolinda ini dhidi ya uhalibifu wa pombe na sumu mbalimbali.
Majani mekundu ya rasberi
Huwa na kiasi kikubwa cha madini chuma yanayosaidia kuimairisha misuli ya kizazi, kuongeza uzalishaji wa maziwa, kupunguza kichefuchefu na maumivu ya uchungu. Hata hivyo imeonekana kwenye baadhi ya tafiti kuwa matumizi kiungo hiki hupunguza madhara yanayoweza kutokea wakati wa kujifungua.
Makundi mengine ya viungo vyenye faida kwa mjamzito
Viungo vingine vyenye faida kwa mjamzito vipo kwenye makundi ya viungo vyenye
Wanga
Nyuzinyuzi
Protini
Mafuta
Vitamin C
Vitamin D na kalisiamu
Vitamin E
Madini chuma
Madini joto
Folate
Orodha ya viungo vyenye virutubisho na madini yaliyoorodheshwa hapo juu inapatikana kwenye Makala ya chakulwa kwa mjamzito.
Viungo hatari kwa mjamito
Baadhi ya viungo ambavyo ni hatari kwa mjamzito endapo vitatumika kwa kiasi kidogo au kikubwa ni;
Mdalasini
Mdalasini hupunguza shinikizo la damu endapo utatumiwana mjamzito. Kama unataka kutumia wakati wa ujauzito, pata ushauri kutoka kwa saktari wako.
Uwatu
Matumizi ya kiungo hiki huweza kusababisha hali ya gesi tumboni, kuongezeka kwa utindikali ndani ya tumbo, kuharisha na ukuaji hafifu wa mtoto kama itatumika kwa kiwango kikubwa.
Fano
Matumizi ya fano kwa kiasi kikubwa ni hatari kwani huwa na homon zinazofanya kazi kama estrogen hivyo kuwa na hatari ya kuongeza mjongeo wa misuli ya uzazi kiasi cha kupelekea mimba kupata uchungu kabla ya wakati
Mbegu hizi ni nzuri kutumika baada ya kujifungua kwa kuongeza uzalishaji wa maziwa au kwa mama asiye mjamzito kutibu matatizo ya kukosa uwiano wa homon
Mnana
Chai yam nana hulegeza kizazi na huweza kuanzisha kutoa mimba kwa kuanzisha uchungu. Matumizi ya mafuta yam nana pia huweza kuamsha uchungu wakati wa ujauzito. Unashauriwa kuepuka matumizi ya kiungo hiki kama una ujauzito.
Kitunguu saumu
Matumizi ya kitunguu saumu ni hatari kwa mjamzito na mara nyingi hakishauriwi kutumika kwa mjamzito. Kitunguu hiki huwa na uwezo wa kusababisha kiungulia na kutokwa na damu kwako na mtoto tumboni.
Kapa
Kiungo hiki huweza kusababisha kuingia hedhi wakati wa ujauzito
Asafetida
Kiungo hiki hakishauriwi kutumika kwa mjamzito kwani huweza kutoa mimba.
Likoris
Kiungo hiki husababisha ongezeko la kemikali ya glycyrrhizin kwenye damu inayozuia ufanyaji kazi za kondo la nyuma ambalo hulisha mtoto na kuleta ongezeko a homon za msongo ambazo ni glukokotikoidi
Anjelika
Kiungo hiki huwa na uwezo mkubwa wa kuyeyusha damu hivyo si salama kutumika wakati wa ujauzito
Ufuta
Tafiti zinaonyesha matumizi ya mbegu za ufuta huwa na uwezo mkubwa wa kuongeza mjongeo wa misuli ya kziazi na hivyo kutoa mimba. Unashauriwa kuepuka kutumia ufuta wakati wa ujauzito. Matumizi wakati wa hatua za mwisho za uchungu au baada ya kujifungua huwa na faida kubwa ya kukata damu haraka.
Madhara ya kula vyakula vyenye viungo vingi
Kula viungo vingi kupita kiasi husababisha
Kiungulia na kucheua tindikali
Maumivu ya tumbo
Kuharisha
Gesi tumboni
Nchi nyingi huwa hazifanyi hivi kuogopa gharama, hata hivyo tafiti nyingi zinashauri ili kuhakiki na kumwepusha mgonjwa na nchi kuingia gharama zaidi kwenye matibabu ya VVU kutokana na majibu yasiyo sahihi.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
7 Oktoba 2021 05:07:03
Rejea za mada hii:
1. ULY CLINIC. Chakula kwa mjamzito. https://www.ulyclinic.com/elimu-kwa-mjamzito-magonjwa/chakula-kwa-mjamzito. Imechukuliwa 07.08.2021
2. Swahili land blogsport. Aina za viungo. http://swahili-land.blogspot.com/2011/05/aina-za-viungo-types-of-spices.html. Imechukuliwa 07.08.2021
3. Mamspresso. What are the spices to eat and avoid during pregnancy. https://www.momspresso.com/parenting/article/what-are-the-spices-to-eat-and-avoid-during-pregnancy. Imechukuliwa 07.08.2021
4. H. Danielewicz, et al. Diet in pregnancy—more than food. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5682869/. Imechukuliwa 07.08.2021
5. Lisha J. John, et al. Herbal Medicines Use During Pregnancy: A Review from the Middle East. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4561638/. Imechukuliwa 07.08.2021