Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Sospeter M, MD
Jumatatu, 23 Agosti 2021

Vyakula vinavyochochea tezi pituitari
Pituitari ni tezi inayofanya kazi ya awali kudhibiti ukuaji wa viumbe. Ili kuongeza kasi ya ukuaji kwa njia asili, tumia vyakula vinavyochochea ufanyaji kazi wake kama vile vyenye vitamin D, E na madini manganese mfano nyama, samaki, mayai, karanga, mboga za majani na nafaka zisizokobolewa.
Ukuaji wa mwili
Ukuaji wa mwili hutegemea uzalishaji wa homon ya ukuaji yenye jina la ‘homon ya ukuaji wa binadamu’ yenye kifupi cha HGH kilichotokana na neno la kiingereza ‘human growth homon’. Homon HGH huzalishwa na tezi ndogo yenye jina la pituitari, tezi hii hufanya kazi kuu ya kuthibiti maendeleo ya ukuaji wa binadamu. Ukuaji wa mwili hujumuisha kuongezeka kwa kimo na umbile la mwili. Ili ukue kimwili na na akili, unapaswa kula vema kuanzia utotoni.
Kula mlo wa kiafya
Kuna faida nyingi za kupata mlo wa kiafya kila siku mbali na kuongeza uzalishaji wa homon za ukuaji. Mlo wa kiafya ni ule uliotokana kwenye makundi matano ya chakula. Baadhi ya vyakula ambavyo vinasisimua tezi pituitari kuzalisha homon ya ukuaji ni;
Mayai
Samaki
Nyanya
Nyama nyeupe kama ile ya kuku
Nyama nyekundu kama ya ng’ombe
Karanga
Zabibu
Komamanga
Raspberi
Mbegu za mustadi(mustard seeds)
Maharagwe ya soya
Vyanzo vya vyakula vyenye vitamin E
Mafuta ya mimea kama alizeti, soya
Karanga kama mfano almond na karanga za kawaida
Mbegu za mimea kama alizeti
Mboga za majani kama spinachi na brokoli
Juisi iliyoongezewa viinilishe
Siagi ya magarini
Vyakula vyenye Vitamin D
Vyakula vyenye vitamin D kwa wingi ni;
Mafuta ya samaki
Nyama nyekundu
Ini
Kiini cha yai
Vyakula vilivyoongezewa viinilishe
Maziwa ya ng’ombe
Vyakula vyenye manganese
Vyakula vyenye manganese kwa wingi
Nafaka zisizokobolewa
Karanga
Soya
Mbaazi
Kunde
Mchele
Mboga za majani
Chai
Viungo vingi vya chakula kama Pilipili manga
Kahawa
Shayiri
Mambo muhimu ya kufahamu
Kula mlo wenye tryptophan kwa wingi pamoja na kujianika kwenye mwanga wa jua la asubuhi huongeza uzalishaji wa homon za ukuaji.
Vyakula vyenye tryptophan kwa wingi ni;
Mayai
Maziwa
Nafaka
Maharagwe
Nyama
Kufunga hupunguza kwa muda mfupi kiasi cha homon insulin mwilini, tendo hili huambatana na kupungua kwa kiasi cha mafuta mwilini pamoja na kuongezeka kwa homon HCG mara 300 zaidi. Ili kuhakikisha kuwa una uzalishaji mkubwa wa homon ya ukuaji wakati wa usiku, punguza kiwango cha homon insulin wakati unalala kwa kuacha kula vyakula vyenye wanga (sukari) kama mkate, wali, ugali na vinywaji vya kusindikwa. Vyakula hivi vimeonekana kuongeza ualishaji wa homon insulin. Kulala usingizi mzito na kwa muda wa kutosha huongeza uzalishaji wa homon ya ukuaji haswa saa moja kabla ya sa sita usiku. Kupata matokeo mazuri, lala masaa mawili kabla ya kuingia katikati ya usiku wa manane.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
7 Oktoba 2021, 05:08:01
Rejea za mada hii:
1. Elitecme. https://www.elitecme.com/resource-center/nursing/improving-endocrine-health-through-a-healthy-diet. Imechukulia 24.08.2021
2. NHI. Manganese. https://ods.od.nih.gov/factsheets/Manganese-HealthProfessional/. Imechukulia 24.08.2021
3. Medline plus. Vitamin E. https://medlineplus.gov/ency/article/002406.htm. Imechukulia 24.08.2021
4. NHS. Vitamin D. https://www.nhs.uk/conditions/vitamins-and-minerals/vitamin-d/. Imechukulia 24.08.2021
5. 6 ways to boost your human growth hormone levels naturally, for better health. https://www.thestar.com.my/lifestyle/health/2020/11/02/boosting-your-human-growth-hormone-levels-naturally-for-better-health. Imechukuliwa 24.08.2021