top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Helen L, M.D

Jumamosi, 30 Januari 2021

Vyakula vyenye uwezo wa kukupa usingizi

Vyakula vyenye uwezo wa kukupa usingizi

Matumizi ya chai ya maua ya pasheni au chamomile, juisi ya tunda damu au kiwi, karanga ya lozi au jozi na nyama ya bata mzinga huchochea kupata usingizi kwa haraka. Endapo una tatizo la kukosa usingizi, tumia moja ya vitu hivyo.


Ni nini huamsha usingizi?


Usingizi huamshwa na homoni yenye jina la 'melatonin' inayozalishwa na tezi 'pineal' iliyopo ndani ya ubongo. Homoni hii hutolewa wakati wa usiku na huitwa kwa jina la 'homoni ya giza'. Kemikali na madini yanayoweza kukufanya uzinzie ni kama apigenin, magnesium na tryptophan. Matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye apigenin, magnesium, tryptophan na melatonin huchochea usingizi kutokana na kuwa au kuongeza uzalishaji wa homoni melatonin.


Vyakula vyenye Apigenin


Vyakula vyenye Apigenin kwa wingi ni kama;


  • Kotimiri (parsley)- tumia majani yake kutengeneza chai

  • Figili (celery)- tumia kama mboga

  • Chai ya Chamomile- tumia majani yake kutengeneza chai

  • Chai ya maua ya pasheni- tumia majani yake kutengeneza chai

  • Rubaruti (Artichokes)- tumia kama chakula


Vyakula vyenye tryptophan


Vyakula vyenye tryptophan kwa wingi ni kama;


  • Lozi (almond)- Tafuna angalau gramu 28

  • Nyama ya bata mzinga(turkey)- kula kama mlo wa usiku


Vyakula vyenye au vinavyosaidia kuzalisha Melatonin


Vyakula vyenye au vinavyosaidia kuzalisha Melatonin ni kama;


  • Matunda damu (tart chery)- tumia kama juisi angalau glasi moja au mbili kabla ya kulala

  • Mayai- tumia mayai mawili kabla ya kulala

  • Maziwa ya ng'ombe- kunywa angalau glasi moja kabla ya kupata usingizi

  • Mafuta au nyama ya samaki- tumia kama mlo au pikia chakula

  • Kiwi- tumia kama tunda au juisi isiyochujwa


Vyakula vyenye magnesium


Vyakula vyenye magnesium kwa wingi ni kama;


  • Lozi- tafuna angalau gramu 28 kabla ya kulala

  • Spinachi ya Vine/spinachi ya kawaida- tumia kama mboga ya majani

  • Mbegu za tikiti- tafuna angalau gramu 28 kabla ya kulala

  • Mbegu za boga- tafuna angalau gramu 28 kabla ya kulala

  • Korosho- tafuna angalau gramu 28 kabla ya kulala

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:41:55

Rejea za mada hii:

1. Bahare Salehi, etal The Therapeutic Potential of Apigenin. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6472148/. Imechukuliwa 28.01.2021
2. Janmejai K Srivastava, etal. Chamomile: A herbal medicine of the past with bright future. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2995283/. Imechukuliwa 28.01.2021
3. Eswar Shankar, etal. Plant flavone apigenin: An emerging anticancer agent. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5791748/#. Imechukuliwa 28.01.2021
4. Sanjeev Shukla, etal. Apigenin: A Promising Molecule for Cancer Prevention. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2874462/. Imechukuliwa 28.01.2021
5. Peir Hossein Koulivand, etal. Lavender and the Nervous System. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3612440/#. Imechukuliwa 28.01.2021
6. Angela Smith Lillehei, etal. Effect of Inhaled Lavender and Sleep Hygiene on Self-Reported Sleep Issues: A Randomized Controlled Trial. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4505755/. Imechukuliwa 28.01.2021
7. Jersey lavender. How to use Lavender Oil For Sleep Problems. https://jerseylavender.co.uk/how-to-use-lavender-oil-for-sleep-problems/. Imechukuliwa 28.01.2021
8. Sleep foundation. The Best Foods to Help You Sleep. https://www.sleepfoundation.org/nutrition/food-and-drink-promote-good-nights-sleep. Imechukuliwa 28.01.2021
9. Cleveland clinic. Magnesium Rich Food. https://my.clevelandclinic.org/health/articles/15650-magnesium-rich-food. Imechukuliwa 28.01.2021
10. Is Tart Cherry Juice Good For Sleep? – Insomnia Buster?. Sleep advisor. https://www.sleepadvisor.org/tart-cherry-juice-sleep/. Imechukuliwa 28.01.2021

bottom of page