top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, M.D

Mhariri:

Dkt. Salome A, M.D

Jumanne, 19 Oktoba 2021

Wastani wa kufa baada ya miaka 10 kwa mwenye VVU

Wastani wa kufa baada ya miaka 10 kwa mwenye VVU

Wastani wa kufa miaka 10 ijayo kutokana na VVU huongezeka sambamba na idadi ya nakala za virusi kwenye damu miezi sita baada ya kuanza ARV. Kuanza ARV mapema na kutumia kwa usahihi hupunguza idadi ya nakala za virusi na kuongeza wastani wa kuishi.


Wastani wa kufa miaka kumi ijayo kwa waliotambulika na VVU kisha kuanzishiwa dawa mapema na kupimwa idadi ya nakala za virusi miezi sita tangu kuanza dawa ulikuwa kama ifuatavyo;


  • Asilimia 13 kwa waliokuwa na virusi nakala 20 kwa mililita moja ya damu

  • Asilimia 14 wa waliokuwa na virusi nakala kati ya 20 hadi 400 kwa mililita moja ya damu

  • Asilimia 20 kwa waliokuwa na virusi nakala kati ya 400 hadi 999 kwa mililita moja ya damu

  • Asilimia 23 kwa waliokuwa na virusi nakala 1,000 au zaidi kwa mililita moja ya damu


Mbali na kutumia ARV kwa usahihi, unapaswa kuhudhulia kliniki kwa kama ulivyopangiwa na daktari wako kwa uchunguzi wa maendeleo yako na tiba na ushauri.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:39:52

Rejea za mada hii:

1. Lee JS et al. Incomplete viral suppression and mortality in HIV patients after antiretroviral therapy initiation. AIDS, online edition. DOI: 10.1097/QAD.0000000000001573 (2017).

bottom of page