top of page

Mwandishi:

Dkt. Adolf S, M.D

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, M.D

Jumapili, 31 Oktoba 2021

Window period ya vipimo vya VVU

Window period ya vipimo vya VVU

Window period ya HIV (dilisha la matazamio) ni muda utakaopita tangu kupata maabukizi ya HIV na kabla ya kugundulika kwa kipimo kwa maambukizi hayo. Muda huu hutofautiana kutegemea aina ya kipimo na mwili wa mtu.


Kila kipimo cha kutambua antibodi kwenye damu huwa na dilisha lake la matazamio. Dilisha la matazamio hutegemea pia aina ya sampuli inayotumika, sampuli ya damu ya kidole au mate mdomoni huwa na dilisha pana la matazamio wakati sampuli ya damu iliyochukuliwa kwenye mishipa huwa na dilisha jembamba la matazamio.


Kuna maswali mawili ya msingi ambayo dilisha la matazamio hujibu ambayo ni:

 • Itachukua muda gani kutambulika na maambukizi ya VVU kwa kipimo baada ya kuambukizwa?

 • Huchukua muda gani kuwa na uhakika wa majibu ya kipimo cha VVU baada ya kuambukizwa?


Je dilisha la matazamio la vipimo vya VVU ni muda gani?


Ni ngumu kusema kwa uhakika ni muda gani dilisha la matazamio linadumu kwa kuwa kuna utofauti kati ya mtu na mtu hivyo, inafanya jibu la swali hili kuwa ni mada ngumu kuifanyia utafiti.


Hata hivyo tafiti moja ilifanyika kuhesabu muda wa dilisha la matazamio kwa vipimo mbalimbali vya haraka vya VVU. Tafiti hii ilitumia damu ya kwenye mishipa.


Uchambuzi wa taarifa za tafiti hii umeonyesha kuwa vipimo vya maabara dalaja la nne vinavyotambua antigeni p24 na antibodi za HIV hutambua maambukizi hayo kati ya wiki 1 hadi 3 ukilinganisha na vipimo vya zamani.


Hata hivyo, taarifa hizo zimeona kwamba, miongozo ya baadhi ya nchi ya kupima maambukizi ya VVU baada ya miezi 3 ili kuthibitisha kutokuwa na VVU ni kuchukua thadhali kubwa isiyo na ulazima.


Vipimo vya maabara dalaja la nne ni vipi?


Vipimo vya maabara dalaja la nne vya kutambua maambikizo ya VVU hutumia sampuli ya damu kutoka kwenye mishipa kutambua uwepo wa antibodi za immunoglobulin G(IgG), IgM na antijeni p24.

Mfano wa vipimo kwenye dalaja la nne ni;

 • Abbott Architect HIV Ag/Ab

 • GS Combo Ag/Ab EIA

 • Siemens Combo HIV Ag-Ab


Vipimo vya haraka dalaja la nne

Kipimo cha haraka daraja la nne ni pamoja ni kama vile Determine HIV-1/2 Ag/Ab Combo


Dilisha la matazamio

 • Dilisha lamatazamio la Vipimo hivi ni kati ya siku 13 mpaka 24. Hii humaanisha kuwa, nusu ya walioambukizwa wanaweza kutambulika kati ya siku 13 hadi 24.

 • Asilimia 99 ya waliopata maambukizi wanaweza kutambulika kuwa wana maambukizi au la ndani ya siku 44

 • Miongozo ya UK imejiwekea dilisha lale la matazamio la vipimo vya daraja la nne kuwa siku 45

 • Dilisha la matazamio la kipimo cha haraka (Determine HIV-1/2 Ag/Ab Combo) hufanana muda wa matazamio na vipimo vya maabara hata hivyo matumizi ya damu ya kidole na mate huwa na dilisha kubwa la matazamio.


Vipimo dalaja la tatu


Vipimo dalja la tatu vingi hutumika kwenye kituo cha kutolea huduma mfano CTC na vituo mbalimbali vya kupima maambukizi. Vipimo hivi hutambua antibodi aina ya immunoglobulin G (IgG) na immunoglobulin M (IgM) na havina uwezo wa kutambua antijeni p24 ya kirusi.


Mfano wa vipimo vya dalaja la tatu

Mfano wa vipimo hivyo ni;

 • INSTI HIV-1/HIV-2

 • Uni-Gold Recombigen HIV tests

 • HIV1/2 SD bioline


Dilisha la matazamio

Dilisha la matazamio la kipimo INSTI ni kama ifuatavyo;


 • Wastani wa dilisha la matazamio ni siku 26 ( wastani wa kati ni siku 22 hadi 31). Hii humaanisha kuwa, nusu ya maambukizi yatatambuliwa kati ya siku 22 hadi 31 baada ya kupata uambukizo.

 • Asilimia 99 ya watu walioambukizwa watatambulika ndani ya siku 50 baada ya kupata maambukizo.

 • Hata hivyo vipimo hivi hutumia damu ya kwenye mishipa, kama damu ya kidole au mate yatatumika, dilisha la matazamio huwa pana zaidi.

 • Miongozo ya UK nan chi zingine imejiwekea dilisha la matazamio ya vipimo hivi kuwa siku 90 kama kipimo kinatumika maeneo yakutolea huduma kwa wateja.


Vipimo vya maabara dalaja la tatu


Hutumika kutambua uwepo wa antibodi za immunoglobulin G (IgG) na immunoglobulin M (IgM). Havina uwezo wa kutambua antijeni p24 ya kirusi cha UKIMWI.


Dilisha la matazamio

Dilisha la matazamio kwa kutumia damu ya mishipa ni wastani wa siku 23. Hata hivyo miongozo ya UK imejiwekea utaratibu wa siku 60.


Vipimo dalaja la pili


Vipimo vingi vya dalaja la pili hutumika maeneo mengi yanayotolea huduma za afya kwa wagonjwa kama CTC, zahanati, hospitali n.k. vipimo hivi hutambua uwepo wa antibodi immunoglobulin G (IgG) na havina uwezo wa kutambua antibodi immunoglobulin M (IgM) au antijeni p24 ya kirusi.


Dilisha la matazamio

Kwa kuwa antibodi IgM na antijeni p24 ya kirusi hutambulika mapema zaidi kuliko antibodi IgG, vipimo dalaja la pili huwa na dilisha pana la matazamio.


Mfano wa vipimo kwenye dalaja la pili ni

 • OraQuick Advance Rapid HIV 1/2

 • Clearview HIV 1/2 STAT-PACK

 • SURE CHECK HIV 1/2


Wastani wa dilisha la matazamio ni siku 31 ( kati ya siku 26 hadi 37). Hii humaanisha kuwa nusu ya maambukizi yatatambuliwa ndani ya siku 26 hadi 37. Asilimia 99 ya maambukizi itabainika kwa vipimo hivi baad aya siku 57.


UK wamejiwekea utaratibu wa dilisha la matazamio la vipimo hivi kuwa siku 90 tangu kupata maambukizi.


Je majibu haya ya muda wa matazamio ya VVU huwa sahihi wakati wote?


Kwa baadhi ya nyakati, majibu ya vipimo hivi yanapaswa kutafsiriwa kwa tahadhali mfano;


 • Kama umetumia damu ya kidole au majimaji kutoka mdomoni kwa kuwa dilisha lake la matazamio huwa pana zaidi

 • Watu wanaotumia PrEP au PEP huchelewa kupata mwitikio wa mwili kutengeneza antibodi hivyo kuongeza dilisha la matarajio.

 • Tafiti hii imefanyika kwa watu wenye HIV-1 aina B, hivyo majibu yanaweza kuwa tofauti dhidi ya virusi aina nyingine vya VVU

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:40:28

Rejea za mada hii:

1. British HIV Association, British Association for Sexual Health and HIV and British Infection Association. Adult HIV Testing Guidelines 2020.

2. Kevin P. et al. Time Until Emergence of HIV Test Reactivity Following Infection With HIV-1: Implications for Interpreting Test Results and Retesting After Exposure, Clinical Infectious Diseases, Volume 64, Issue 1, 1 January 2017, Pages 53–59, https://doi.org/10.1093/cid/ciw666

3. Delaney KP et al. Time from HIV infection to earliest detection for 4 FDA-approved point-of-care tests. https://www.croiconference.org/abstract/time-hiv-infection-earliest-detection-4-fda-approved-point-care-tests/. Imechukuliwa 31.10.2021

4. Avert. How do hiv tests work and what's involved?. https://www.avert.org/hiv-testing/whats-involved. Imechukuliwa 31.10.2021

bottom of page