Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Benjamin L , MD
Jumatano, 25 Agosti 2021

Zinki na manii
Zinki huchochea uzalishaji wa homon testosterone, huongeza ubora wa manii na kupunguza hatari ya ugumba kwa mwanaume. Unaweza kupata zinki kwa wingi kwa kula nyama, samaki, mayai na uduvi.
Ni nani anaweza faidika na zinki?
Mwanaume anayeweza kupata faida kwa kutumia zinki ni yule mwenye;
Ugumba kutokana na Upungufu wa zinki
Mwenye uwezo mdogo wa kuzalisha manii kutokana na upugnufu wa zinki
Mwanaume gani hawezi faidika kwa kutumia zinki?
Mwanaume ambaye hawezi faidika kwa kutumia madini zinki hata kama atatumia kwa wingi ni yule;
Asiye na uwezo wa kuzalisha manii
Mwenye madhaifu ya umbile la manii
Ubora wa manii ni nini?
Ubora wa manii huchangia uwezo wake wa kupita ukeni kisha kusafiri kwenye mirija ya uzazi ili kufanya utungisho wa yai.
Vitu vinavyoashiria ubora wa manii
Umbile la manii
Uwezo wa kujongea
Idadi ya manii
Mambo gani yasiyofanywa na madini zinki
Mambo ambayo madini zinki haiwezi kufanya ni;
Kuamsha uzalishaji wa manii kwa mwanaume asiyezalisha manii( mgumba)
Kuboresha umbile la manii kwa mwenye tatizo la umbile la manii
Kuboresha uwezo wa kujongea kwa manii kwenye manii isiyojongea
Njia zingine za kuimarisha ubora wa manii
Mambo mengine ya kufanya ili kuongeza idadi ya manii ni;
Kufanya mazoezi
Kuacha msongo wa mawazo
Kuacha uvutaji sigara kama unafanya hivyo
Kuacha dawa za kulevya kwa watumiaji
Kula mlo kamili kutoka kwenye makundi matano ya chakula
Vyakula gani vyenye zinki kwa wingi?
Zinki ni madini hupatikana kwenye vyakula kama;
Nyama
Samaki
Mayai
Samaki wenye magamba kama uduvi, kaa n.k
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
7 Oktoba 2021 05:09:22
Rejea za mada hii: