Vidonda vya homa mdomoni-cold sores
​
Imeandikwa namadaktari wa uly clinic
​
Utangulizi
​
Vidonda vya homa mdomoni kwa jina jingine hufahamika kama cold sores ni maambukizi yanayosababishwa na virusi . Hutokea kama vidonda vidogo vilivyo jaa maji kwenye midomo yaani malengelenge. Malengelenge haya hukusanyika pamoja. Baada ya malengenge kupasuka hutengeneza gamba. Vidonda baridi mdomoni mara nyingi huchukua wiki mbili hadi nne kupona kabisa bila kuacha kovu.
Vidonda baridi mdomoni huambukizwa kutoka mtu mmoja na mwingine kwa kuwa na mgusano na mtu mwenye tatizo hili kama vile njia ya kubusiana/busu la mdomoni. Husababishwa na kirusi kinachoitwa herpes simplex-1 (HSV-1) ambaye hufanana na kirusi anayesababisha tatizo kama hili kwenye sehemu za siri yaani herpes simplex virus 2(HSV-2).
Virusi hawa wote huweza kusababisha maambukizi kwenye maeneo ya siri ama na kwenye midomo, na huambukizwa kwa njia ya ngono ya mdomoni. Vidonda baridi huambukizwa hata kama huna vidonda.
Hakuna tiba kwa ajili ya vidonda baridi mdomoni na vidonda baada ya kupona vyenyewe huweza kujirudia.
Vidonge dhidi ya virusi huweza kusaidia kuponyesha vidonda baridi mdomoni kwa haraka na huweza kupunguza kwa ugonjwa kujirudia rudia.
Dalili, Visababishi, Vihatarishi, Madhara, Vipimo na matibabu, Pata tiba na madaktari wa ulyclinic
​
Wasiliana na daktari wa Ngozi wa ULY CLINIC kupata tiba kwa kubonyeza hapa au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.