top of page

Imeandaliwa na madaktari wa ULY-Clinic

 

 

 

Kuongezeka vimengenya vya ini kwenye damu

​

Kuongezekakwa vimengenya vya ini kwenye kipimo cha damu huweza kuonyesha kuwa kuna uharibifu kwenye chembe hai za ini. Chembe zilizoungua au kujeruhiwa huvujisha kiwango kikubwa cha kemikali Fulani katika damu zikiwemo vimengenya ambavyo hupelekea wingi viwango vyake kupanda sana.

 

Vimengenya bayana ambavyo hupanda wakati ini limejeruhiwa huwa ni;

 

  • Alanine transaminase (ALT)

  • Aspartate transaminase (AST)

 

Kupanda kwa vimengenya vya ini huweza kutambuliwa kwenye vipimo vya desturi vinavyofanyika hospitali. Wakati mwingi vimengenya vinavyotolewa na ini huwa vimepanda kidogo kwa kipindi cha mpito, mara nyingi pia haimaanishi kuna ugonjwa sugu ndani ya ini ama kuna tatizo kubwa.

 

Visababishi

 

Hali na magonjwa mengi huweza kuchangia kuongezeka kwa viwango vya vimengenya vya ini kwenye damu. Ukiwa hospitali daktari wako atafanya  uchunguzi wa histolia ya ugonjwa wako na kutambua nini kilichochosababisha.

 

Baadhi ya mambo yanayosababisha kwa kiwango kikubwa ni kama vile;

 

  • Madawa Fulani, kama dawa aina ya statin ambayo hudhibiti kiwango cha lehamu kwenye -simvastatin atovarstatin n.k

  • Unywaji wa pombe

  • Moyo kufeli

  • Homa ya manjano inayosababishwa na kirusi cha hepatitis A

  • Homa ya manjano inayosababishwa na kirusi cha hepatitis B

  • Homa ya manjano inayosababishwa na kirusi cha hepatitis C

  • Ini kuwa na mafuta mengi- kusikotokana na pombe

  • Unene sana- kitambi

  • Madawa baridi ya kupunguza maumivu kama panadol

 

Sababu zingine ni;

 

  • Michomo ya ini kutokana na pombe-

  • Michomo kwenye ini kutokana na shambulio la kinga za mwili

  • Uharibifu wa utumbo mwembamba kutokana na protin ya gluten

  • Makovu kwenye ini- cirrhosis

  • Maabukizi ya Kirusi cha cytomegalovirus

  • Kirusi cha epistein Barr

  • Michomo kwenye kifuko cha nyongo

  • Kushikwa kwa moyo

  • Kiwango kikubwa cha madini chuma kwenye damu

  • Kiwango cha chini cha homoni thyroid

  • Saratani ya ini

  • Mononucleosis

  • Michomo kwenye kongosho

  • Michomo kwenye misuli ama ngozi

  • Sumu ama dawa kwenye ini

  • Ugonjwa wa Wilsons(kiwango kikubwa cha madini ya copper mwilini)

​

Imeboreshwa 11/11/2018

Imechapishwa 3/3/2015

bottom of page