Vipimo vya maabara
Katika kurasa hii utafahamu kuhusu vipimo mbalimbali, namna vinavyofanyika, kwanini vinafanyika na majibu pia yanasomwa vipi. Ukurasa huu ni maalumu kwa ajili ya wagonjwa tu.

Kipimo cha Endoskopi
Ni kipimo salama na muhimu kinachosaidia kuona moja kwa moja ndani ya umio, tumbo na duodenamu ili kubaini chanzo cha dalili kama maumivu ya chembe ya moyo, kiungulia, vidonda vya tumbo na kutokwa damu kwenye mfumo wa juu wa chakula. Ingawa kinaweza kuwa na madhara machache, kufanyika kwa tathmini sahihi na wataalamu husaidia kugundua magonjwa mapema na kupata matibabu yanayofaa.

Kipimo cha glukosi
Kipimo cha glukosi hutumika kutambua kiwango cha sukari ya glucose kwenye damu. Mgonjwa mwenye dalili ya kupoteza fahamu, kukojoa mara kwa mara, kiu ya mara kwa mara na njaa ya mara kwa mara atafanyiwa kipimo hiki kutambua kama dalili hizo zinahusiana na sukari na pia kuchunguza ufanisi wa matibabu anayopata mgonjwa wa kisukari n.k


