Mwandishi:
Mhariri;
Dkt. Sima, CO
Dkt. Lugonda B, MD
Ijumaa, 3 Septemba 2021
Kipimo cha muda wa prothrombin
Kipimo cha muda wa prothrombin kinauwezo wa kutambua muda gani damu itaganda baada ya kupatwa na jeraha mwilini au kwenye mishipa ya damu. Utambuzi wa muda huo humwezesha daktari kufahamu maradhi na madhara ya matibabu au dawa zinazoathiri uwezo wa damu kuganda.
Kwa kawaida damu inatakiwa ganda ndani ya sekunde 10 hadi 13 kwa mtu ambaye hajanywa dawa za kugandisha damu na kwa mtu aliyekunywa dawa za kugandisha damu huchukua sekunde 2 hadi 3.5
Kipimo cha muda wa Prothrombine kinaweza onyesha tatizo la damu kuchelewa ganda kama mgonjwa ana maradhi ya;
Upungufu wa Vitamin K
Ini
Upungufu wa protini zinazogandisha damu
Vinywaji
Vinywaji au vyakula vinavyoweza athiri kipimo cha muda wa Prothrombin na kupelekea damu kuwahi kuganda ni;
Pombe
Nyama ya ng’ombe
Ini la nguruwe
Chai ya kijani
Maharage ya soya
Kipimo hiki ni nini?
Kipimo cha muda wa hufanya kazi kwa kuangalia uwezo wa damu kuganda kwa kutumia protini ya ugandishaji damu yenye jina la prothrombin. Prothrombin ni aina ya protini inayozalishwa na ini na hufanya kazi ya kugandisha damu.
Umuhimu wa kipimo
Kipimo cha muda wa Prothrombin hufanyika kwa lengo la kutambua muda ambao damu itachukua kuganda.
Mgonjwa gani anapaswa kufanya kipimo hiki?
Kipimo cha muda wa prothrombini hufanyika kwa wagonjwa mwenye magonjwa au hali zifuatazo;
Kutumia dawa za kuyeyusha damu kama warfarin
Kutokwa na damu bila sababu
Kuchubuka au kupata majeraha kirahisi
Kutokwa na damu puani
Fizi kutoa damu
Kuganda kwa damu kwenye vein na ateri
Ugonjwa mkali wa ini
Hitaji la kufanyiwa upasuaji
Aina ya sampuli inayotakiwa
Damu ya kwenye mshipa au kidole hutumika kama sampuli ya kupima kipimo hiki, kiasi cha damu kinachoweza kuchukuliwa ili kuhifadhiwa huwa kati ya mililita 4 hadi 10 tu.
Namna ya kukusanya sampuli
Mhudumu wa afya atachukua sampuli ya damu kwenye kidole na kuiweka kwenye kipimo kisha kuongeza kemikali ambayo itasaidia kugundua ni muda gani damu itachukua kuganda .
Kwa wanawake
Ukusanyaji wa sampuli hufanana kama ilivyoainishwa hapo juu
Kwa wanaume
Hakuna utofauti wa ukusanyaji wa sampuli kati ya mwanamke na mwanaume
Ukusanyaji wa sampuli kwa njia zingine
Hakuna sampuli mbadala wa damu inayoweza kutumika kwa ajili ya kipimo hiki mbali na damu
Utunzaji wa sampuli
Sampuli ya moja kwa moja kutoka kwenye kidole inaweza tumika kupima kipimo hiki hapohapo hivyo kutohitaji hifadhiwa au subiria majibu. Sampuli ya damu pia inaweza chukuliwa kwenye mshipa mkuu mkubwa wa damu na kuhifadhiwa kwenye tube ya bluu au pinki yenye kemikali za kuzuia damu kuganda kisha kuhifadhiwa kwenye jokofu na kufanyiwa vipimo ndani ya masaa 24.
Muda wa sampuli kuwa hai
Sampuli ya kidole cha mkono inapaswa kufanyiwa kazi mara baada ya kutolewa maana huganda kirahisi inapopatwa na hewa. Damu kutoka kwenye mishipa inaweza hifadhiwa kwenye tube ya rangi ya bluu au pinki ( zina kemikali ya sodium citrate inayozuia damu kuganda) kisha kuwekwa kwenye jokofu katika nyuzi joto 4 za sentigredi na kufanyiwa kazi ndani ya masaa 24
Muda wa kupata majibu ya kipimo chako
Unaweza kupata majibu ndani ya dakika chache kama damu imechukuliwa kwenye kidole au kusubiria kwa muda wa nusu saa au zaidi kama damu imechukuliwa kwenye mishipa ya damu kwa ajili ya kupima baadae
Usomaji wa majbu
Kuna majibu ya aina mbili, majibu chanya yanayotokea kama damu inaganda baada ya muda wa kawaida ( inachelewa ganda) na majibu hasi ambayo hutokea kama damu itaganda ndani ya muda wa kawaida au pungufu ya muda wa kawaida.
Majibu chanya
Majibu chanya kwa mgonjwa mwenye tatizo la kuchelewa ganda kwa damu huwa chanya endapo damu inaganda muda mrefu zaidi ya kawaida au muda mfupi zaidi ya kawaida.
Magonjwa yanayoongeza muda wa prothrombin(kufanya damu ichelewa genda) ni;
Ugonjwa wa ini
Upungufu wa vitamin K
Upungufu wa vigandisha damu kama (Fakta II, VII, IX, na X )
Matumizi ya dawa za kupinga ufanyaji kazi wa vitamin K kama warfarin
Sindromu ya antibodi za antiphospholipid
Msambao wa kuganda damu ndani ya mishipa ya damu (DIC)
Kupungua kwa muda wa prothrombin au kuganda kwa damu chini ya muda wa kawaida humaanisha;
Unakunywa kwa wingi vidonge vya vitamin K kwa wingi
Kula vyakula vyenye vitamin K kwa wingi
Umefunga kula. Kufunga hupunguza fakta II, VII na X kwenye damu na
Majibu hasi
Majibu hasi hutokea pale endapo muda wa damu kuganda ni ndani ya sekunde 10 hadi 13
Ushauri wa msingi kwa mgonjwa
Dawa ambazo zinaweza kuathiri kipimo cha muda wa Prothrombin ni;
Dawa jamii ya Barbiturates
Vitamin K
Vidonge vya uzazi wa mpango
Argatroban
Dabigatran
Rivaroxaban
Apixaban
Edoxaban
Mambo yanayoweza athiri muda wa damu kuganda
Kuhifadhiwa kwa damu kwa muda mrefu
Kutofungwa vema kwa chupa ya kuhifadhiwa damu
Kuwa na kiwango kikubwa cha kolestrol kwenye damu
Kuwa na damu nyingi
Madhara ya kipimo
Maumivu kwenye sehemu damu ilipotolewa, kupata bruizi na kutokwa na damu
ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyte ile ya kiafya.
ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyte ile ya kiafya.
Imeboreshwa,
8 Novemba 2021 10:44:39
Rejea za mada hii
1. MedScape. Prothrombin Time. https://emedicine.medscape.com/article/2086058-overview , Imechukuliwa 18/8/2021
Health Line. Prothrombin Time. https://www.healthline.com/health/prothrombin-time-pt, Imechukuliwa 18/8/21
PubMed. Prothrombin Time. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/31334989/ , Imechukuliwa 18/8/21
WHO. Prothrombin Time. https://www.who.int/bloodproducts/publications/TRS_979_Annex_6.pdf. Imechukuliwa 18/8/21
CDC. Prothrombin Time. https://www.cdc.gov/ncbddd/hemophilia/diagnosis.html , Imechukuliwa 18/8/2021
V. Rimac, et al. Is it acceptable to use coagulation plasma samples stored at room temperature and 4°C for 24 hours for additional prothrombin time, activated partial thromboplastin time, fibrinogen, antithrombin, and D-dimer testing?. https://onlinelibrary.wiley.com/doi/full/10.1111/ijlh.12664. Imechukuliwa 03.09.2021
Blood Collection Tubes. https://www.labce.com/spg263741_blood_collection_tubes.aspx. Imechukuliwa 03.09.2021
L V Rao, et al. Stability of prothrombin time and activated partial thromboplastin time tests under different storage conditions. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/10958859/. Imechukuliwa 03.09.2021
Mayoclinic. Prothrombin time test.https://www.mayoclinic.org/tests-procedures/prothrombin-time/about/pac-20384661. Imechukuliwa 03.09.2021
Rocky Yang, et al. Prothrombin Time. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK544269/. Imechukuliwa 03.09.2021