Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Mangwella S, MD
Dkt. Benjamin L, MD
24 Agosti 2026, 03:43:15

Chai ya ndizi mbivu
Kwa kula ndizi mbivu utapata virutubisho kama vitamin B6, potassium, magnesium, manganese na shaba. Hata hivyo chai ya ndizi mbivu na maganda yake huwa na vitamin B6, potassium na tryptophan kwa wingi kiasi cha kuweza kukupa usingizi, kuthibiti shinikizo la damu na kuondoa sumu mwilini.
Chai ya ndizi
Chai ya ndizi hutengenezwa kwa kuchemsha vipande vya ndizi iliyosafishwa vema kwenye maji kisha kuvitoa na kunywa maji yake. Chai hii inaweza tengenezwa kwa kutumia ndizi iliyomenywa au isiyomenywa. Chai ya ndizi isiyomenywa huhitaji muda mrefu kupikwa kutokana na kuwa na nyuzinyuzi nyingi, hata hivyo huwa na virutubisho vingi zaidi haswa vitamin B6 na potassium. Unaweza tia mdalasini au asali ili kuongeza radha, lakini pia unaweza kunywa bila kuweka viungo hivyo.
Kwa ujumla chai ya ndizi huwa na baadhi ya virutubisho vifuatavyo;
Vitamin B6
Potassium
Magnesium
Manganese
Copper
Nishati kidogo
Virutubisho ambavyo hupotea kwa kutengeneza chai ya ndizi ni Vitamin C. Kwa kutumia cha ya ndizi unapata faida zifuatazo;
Kuondoa sumu mwilini
Huondoa gesi tumboni
Huimarisha usingizi
Huimarisha afya kwa ujumla
Huondoa sumu mwilini
Kutokana na kuwa na na viuaji sumu asilia kama dopamine na gallocatechin vinavyoondoa sumu mwilini, kunywa chai ya ndizi huweza kukukinga na magonjwa sugu kama vie maradhi ya moyo na mishipa ya damu. Ili kupata faida zaidi, kunywa chai ya ndizi yenye maganda yake.
Kupunguza hatari ya kupata magonjwa sugu
Madini potassium na magnesium yameonekana kwenye tafiti mbalimbali kupunguza kwa asilimia 27 zaidi hatari ya kupata shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na mishipa ya damu kama vile kiharusi. Ili kufata zaidi hizi, utapaswa kutumia mara kwa mara chai hii.
Huimarisha usingizi
Chai ya ndizi ina virutubisho vya potassium, magnesium na tryptophan kwa wingi ambavuo hufanya kazi nzuri yakukupa usingizi haraka na wa muda mrefu. Hufanya kazi hiyo kwa kulegeza misuli, kuongeza uzalishaji wa homon melatonin, ni homon muhimu ya usingizi.
Huondoa gesi tumboni
Kwa kuwa ina madini potassium kwa wingi yanayosaidia kurekebisha uwiano wa maji, shinikizo la damu na madini mwilini, kutumia chai ya ndizi huondoa tatizo la gesi tumboni kutokana na kupotea kwa uwiano wa chumvi na maji. Hufanya hivi kwa kuongeza utolewaji wa madini chumvi kupitia mkojo.
Hatua za kuandaa chai ya ndizi isiyo na maganda
Weka maji vikombe viwili hadi vitatu kwenye sufuria ya kuchemshia chai kisha yachemshe
Menya ndizi yako kisha ondoa vipande vya mwishoni
Weka ndizi kwenye maji yanayochemka
Punguza moto kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5 hadi 10
Ongeza mdalasini na asali (kama utapenda)
Ondoa ndizi kisha weka chai yako kwenye kikombe tayari kwa kunywa kunywa(unaweza hifadhi chai iliyobaki kwenye chupa ila isikae zaidi ya masaa 24)
Hatua za kuandaa chai ya ndizi yenye maganda
Weka maji vikombe viwili hadi vitatu kwenye sufuria ya kuchemshia chai kisha ya chemshe
Safisha ndizi yako kwenye maji safi yanayotiririka kuondoa uchafu wote na kemikali zisizotakiwa
Ondoaa miishio yake kisha kata iwe kwenye vipande viwili
Weka vipande hivyo kwenye maji yanayochemka
Punguza moto ili ichemke na moto mdogo kwa muda wa dakika 15 hadi 20 6. Ongeza mdalasini na asali kama utapenda
Ondoa ndizi kwenye chai yako kisha weka chai yako kwenye kikombe na kuinywa (unaweza kuhifadhi chai iliyobaki kwenye chupa ila isikae zaidi ya masaa 24)
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
