Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Sospeter M, MD
Dkt. Salome A, MD
2 Aprili 2026, 16:17:51

Dalili za hatari kwa kichanga
Dalili za hatari
Mtoto anapokuwa anachunguzwa na mtaalamu wa afya (dakitari) kwa kawaida lazima kuuliza dalili za hatari kwa mlezi wake kama hizi zifuatazo;
Kutapika kila kitu anapokuwa analishwa
Kushindwa kula au kunyonya
Kupata degedege kwa ugonjwa alionao
Kuchoka sana ama kutepweta
Kupoteza fahamu
Dalili zinazohitaji huduma ya haraka sana
Mtoto kutopumua vema ama kutopumua kabisa
Kuwa wa na rangi ya bluu kenye ulimi hasa chini ya ulimi ama ngozi za midomo
Kuzimia
Kupata dalili za shock kama mikono kuwa ya baridi, damu kwenye kucha kutorudi haraka baada ya kubonyeza, kuwa na mapigo ya moyo ya haraka na mdundo mdogo wa mishipa ya damu, na shinikizo la damu la chini ama lisilopimika kabisa
Dalili za mtoto kupoteza maji kwa kiwango cha juu kwa mtoto anayehara kama vile kuchoka sana, macho kuzama ndani, ngozi kuvutika na kutojirudia haraka
Kama dalili hizi zipo kwa mtoto wako tafadhari mfikishe mtoto mapema hospitali na hata kama kuna foleni omba msaada ili mtoto apate huduma za haraka kuepuka kupoteza uhai
Dalili za kupewa kipaumbele kwenye matibabu na dakitari
Mtoto mdogo yaani mtoto anayeumwa na yupo umri chini ya miezi miwili
Joto mwili kupanda yaani mtoto anajoto kali sana
Jeraha ama kuwa na ugonjwa unaohitaji matibabu ya upasuaji wa haraka
Upungufu wa damu unaoonekana kwa kuwa mweupe chini ya kope za macho hasa kope ya chini na ulimi
Kula ama kunywa sumu
Maumivu makali
Upumuaji wa shida
Kuchoka kulialia ama kulia anaposhikwa ama kuchoka
Mtoto aliyepewa rufaa
Utapiamlo mkali unaohushisha kukonda sana kunakoonekana
Kuvimba miguu yote kunakotokana na maji
Michomo mibaya (kuungua vibaya)
Mtoto ambaye anashindwa kula ama kutapika kila kitu anacholishwa hatakuwa na uwezo wa kunywa dawa na hupoteza maji kwa wingi na hivyo kupungukiwa maji mwilini. Haijalishi ni nini kimesababisha hali hiyo, mtoto huyu hawezi kutibiwa nyumbani la sivyo ataendelea kuwa na hali mbaya kila kukicha.
Mtoto akipata degedege au kuchoka sana huwa maranyingi anaumwa sana na huenda anamaambukizi ya kwenye kuta za ute wa mgongo kwa jina jingine homa ya uti wa mgongo.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
