Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Sospeter B, MD
Dkt. Salome A, MD
2 Aprili 2026, 16:17:51

Dalili zinazoambatana na kuota meno
Idadi kadha ya dalili za magonjwa kwa watoto wa umri wa kuota meno zimekuwa zikihusianishwa na kuota meno enzi na enzi, wakati huo tiba kadhaa asili zimekuwa zikipendekezwa na si zote ni salama.
Â
Tafiti hii inatoa kumbukumbu na uthibitisho wa dalili na viashiria kiasi vinavyoambatana na kuota meno ya kwanza.Â
Uzuri wa utafiti huu ni umefanyika kwa kufuatilia watoto kabla ya kuota meno na kufanyika kwa zaidi ya miezi kadhaa na kuhusisha watoto zaidi ya 100 wenye afya njema. Sampuli ilipatikana kwa kutumia kikokteo cha nguvu.
Matokea ya utafiti
Tafiti ilirekodi joto la sikio pamoja na dalili zilizokuwa zinatokea wakati wa kipindi cha kuota meno ya mbele. Dalili zifuatazo zilionekana kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na kuota meno ya chini katika kipindi cha miezi 4 hadi 6.
Kujing’ata
Kutokwa udenda
Kujikuna fizi
Kunyonya
Kutotulia
KutolalaÂ
Kukuna masikio
Kukosa hamu ya kula
Harara usoni
Ongezeko kiasi la joto kufikia nyuzi joto 39
Â
Hitimisho
Dalili nyingi za wastani zilizofikiriwa hapo awali kuambatana na kuota menozimeonekana katika tafiti hii kuhusiana kwa muda mfupi. Hakuna mkusanyiko wa dalili hata hivyo unaotegemewa kutabiri uchomozaji wa meno. Kabla ya mzazi kuhusianisha uotaji meno na dalili aliyonayo mtoto, ni muhimu kufikiria na kuondoa sababu zingine za hatari zinazoweza kupelekea dalili hizo.
Wapi unaweza kupata makala zaidi?
Soma zaidi kuhusu makala ya na makala zingine za uhusiano wa dalili husika na kuota meno. Baadhi ya viungo ni :
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
