Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
2 Aprili 2026, 15:48:01

Dawa za kusafisha kizazi baada ya kutoa mimba kwa dawa ni zipi?
Baada ya kutoa mimba kwa kutumia dawa (kama misoprostaol), watu wengi huuliza: “Je, kuna dawa ya kusafisha kizazi?” Hili ni swali muhimu kwa sababu linahusiana moja kwa moja na afya ya uzazi na usalama wa mwanamke.
Katika makala hii, utapata maelezo ya kina kuhusu:
Dawa zinazotumika
Jinsi zinavyofanya kazi
Dalili za kizazi kutosafika vizuri
Lini unapaswa kumuona daktari
Je, “kusafisha kizazi” ni nini?
“Kusafisha kizazi” humaanisha kuondoa mabaki yoyote yaliyobaki ndani ya mfuko wa uzazi (uterus) baada ya mimba kutoka. Mabaki haya yanaweza kusababisha:
Maambukizi
Kutokwa damu kupita kiasi
Maumivu ya tumbo
Dawa zinazotumika kusafisha kizazi
1. Misoprostol
Hii ndiyo dawa kuu inayotumika.
Jinsi inavyofanya kazi:
Husababisha mfuko wa uzazi kusinyaa (contractions)
Husaidia kutoa mabaki yaliyobaki ndani ya kizazi
Matumizi yake:
Hutumika peke yake au baada ya kutumia dawa nyingine ya kutoa mimba
Mara nyingi hutolewa kwa maelekezo ya daktari
2. Mifepristone
Hutumika pamoja na Misoprostol.
Kazi yake:
Huzuia homoni ya projesteroni
Husaidia kuandaa kizazi kutoa mimba kikamilifu
Hupunguza uwezekano wa mabaki kubaki ndani ya kizazi.
3. Antibayotiki (dawa za maambukizi)
Hizi si za kusafisha moja kwa moja, lakini hutolewa ikiwa:
Kuna dalili za maambukizi
Kuzuia infection baada ya utoaji mimba
Dalili za kizazi kutokusafika vizuri
Baada ya kutoa mimba kwa dawa, angalia dalili hizi:
Kutokwa damu nyingi sana (kubadilisha pedi iliyojaa kila saa)
Maumivu makali ya tumbo yasiyopungua
Homa
Harufu mbaya kutoka ukeni
Kutokwa damu kwa muda mrefu (zaidi ya wiki 2–3)
Hizi zinaweza kuashiria kuwa mimba haijakamilika kutoka (mimba isiyokamilika kutoka)
Nini kifanyike kama kizazi kakijasafika?
Ikiwa dawa hazijasaidia kikamilifu, daktari anaweza:
Kutoa dozi nyingine ya Misoprostol au
Kufanya usafishaji wa kitaalamu (wa kufyonza masalia kutoka kwenye kizazi kwa upasuaji mdogo) na
Kukupa antibayotiki ili kuzuia maambukizi
Mambo muhimu ya kuzingatia
Usitumie dawa bila ushauri wa daktari. Matumizi mabaya yanaweza kusababisha:
Kutokwa damu nyingi
Maambukizi kwenye kizazi
Madhara makubwa ya kiafya
Mimba kutokamilika kutoka
Kila mwili ni tofauti
Watu wengine:
Kizazi hujisafisha kabisa bila dawa ya ziada
Wengine huhitaji matibabu zaidi
Ufuatiliaji ni muhimu
Ni vyema:
Kufanya uchunguziwa ultrasound ikiwa inawezekana
Kufuatilia dalili zako kwa makini
Lini umuone Daktari haraka?
Muone daktari mara moja ikiwa:
Unavuja damu nyingi sana
Una homa kali
Una maumivu makali yasiyopungua
Unahisi kizunguzungu au udhaifu mkubwa
Hitimisho
Dawa ya kusafisha kizazi baada ya kutoa mimba kwa dawa mara nyingi ni Misoprostol, ambayo husaidia mfuko wa uzazi kujisafisha kwa kusinyaa na kutoa mabaki yaliyobaki. Hata hivyo, si kila mtu anahitaji dawa ya ziada, na ni muhimu kupata ushauri wa daktari ili kuepuka madhara.
Rejea za mada hii:
World Health Organization. Abortion care guideline. Geneva: World Health Organization; 2022.
World Health Organization. Medical management of abortion. Geneva: World Health Organization; 2018.
American College of Obstetricians and Gynecologists. Medication abortion up to 70 days of gestation. Practice Bulletin No. 225. Obstet Gynecol. 2020;136(4):e31–e47.
International Federation of Gynecology and Obstetrics. Misoprostol recommended regimens 2017. London: FIGO; 2017.
Raymond EG, Grossman D, Mark A, Upadhyay UD, Dean G, Creinin MD. Commentary: No-test medication abortion: A sample protocol for increasing access during a pandemic and beyond. Contraception. 2020;101(6):361–366.
Royal College of Obstetricians and Gynaecologists. The care of women requesting induced abortion. London: RCOG; 2011 (updated guidance available).
Kulier R, Kapp N, Gülmezoglu AM, Hofmeyr GJ, Cheng L, Campana A. Medical methods for first trimester abortion. Cochrane Database Syst Rev. 2011;(11):CD002855.
National Abortion Federation. Clinical Policy Guidelines. Washington, DC: NAF; 2022.
Centers for Disease Control and Prevention. Abortion surveillance — United States. MMWR Surveill Summ. 2021.
Williams Obstetrics. Cunningham FG, Leveno KJ, Bloom SL, et al. 26th ed. New York: McGraw-Hill; 2022.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 14:07:30
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
