top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

2 Aprili 2026, 16:07:08

Je, mimba huonekana kwenye kipimo cha mimba kuanzia siku ngapi?

Kipimo cha Mkojo


Huonyesha:

  • Uwepo wa mimba ikiwa kuna homoni ya ujauzito (human chorionic gonadotropin).

  • Huwezi kuona kiinitete au mfuko wa ujauzito.


Kinaweza kugundua mimba lini?

  • Kuanzia siku 7-14 baada ya upvuleshaji  (au siku 1-5 baada ya kukosa hedhi).


Kipimo cha Damu


Huonyesha:

  • Kiwango sahihi cha homoni ya mimba, ambacho kinaweza kutumika kukadiria umri wa ujauzito.

  • Homoni ya ujauzito inaweza kusaidia kuthibitisha ujauzito hata kabla ya kuonekana kwenye kipimo cha ultrasound.


Kipimo kinaweza kugundua mimba lini?

  • Kuanzia siku 6-8 baada ya uovuleshaji (kabla ya kukosa hedhi).


Kipimo cha Ultrasound

Kuna aina kadhaa za vipimo vya Ultrosound kwa ajili ya kutambua mimba ambavyo ni;


Ultrasound ya Uke

Huonyesha kulingana na umri wa ujauzito:

Wiki ya Ujauzito

Kinachoonekana kwenye Ultrasound ya Uke

Wiki 4-5 (Siku 28-35)

Gestational sac (mfuko wa ujauzito) unaweza kuanza kuonekana.

Wiki 5-6 (Siku 35-42)

Yolk sac (mfuko wa lishe kwa kiinitete) huanza kuonekana.

Wiki 6-7 (Siku 42-49)

Kiinitete (embryo) na mapigo ya moyo yanaweza kuonekana kwa mara ya kwanza.

Wiki 8-9 (Siku 56-63)

Kiinitete kinakuwa na umbo dhahiri, vichipukizi vya mikono na miguu vinaweza kuonekana.

Wiki 10-12

Mtoto anaonekana akiwa na viungo vyake vikiwa vimeanza kuunda.


Mimba inaweza kuonekana lini?

  • Kuanzia wiki ya 4-5 na kuendelea.


Ultrasound ya Tumbo

Huonyesha mimba kulingana na umri wa ujauzito kama ifuatavyo;

Wiki ya Ujauzito

Kinachoonekana kwenye Ultrasound ya Tumbo

Wiki 5-6

Inaweza kuanza kuonyesha gestational sac, lakini si mara zote.

Wiki 6-7

Yolk sac na kiinitete (embryo) vinaweza kuonekana.

Wiki 7-8

Mapigo ya moyo ya mtoto yanaweza kuonekana kwa uwazi.

Wiki 9-12

Mtoto anaonekana kwa uwazi zaidi, na viungo vikuu vinaweza kutofautishwa.

Mimba inaweza kuonekana lini?

Katika kipimo cha ultrosound ya tumbo, mimba huanza kuonekana kuanzia wiki ya 5-6 na kuendelea.


Hitimisho

Mimba inaweza kuthibitishwa kwenye kipimo cha mkojo au damu kabla ya kuonekana kwenye ultrasound. Mfuko wa ujauzito (gestational sac) huanza kuonekana wiki ya 4-5, kiinitete (embryo) huanza kuonekana wiki ya 5-6 wakati mapigo ya moyo huonekana kwa mara ya kwanza wiki ya 6-7. Kwa kutumia ultrasound ya tumbo, mimba huonekana baadaye kidogo kuliko ultrasound ya uke.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 16:07:08

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

bottom of page