Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Charles W, M.D
24 Agosti 2026, 03:43:15

Kiasi cha maji ya kunywa kila siku kwa watoto
Watoto wanapaswa kunywa maji vikombe 2 hadi 8 vya chai kwa siku huku wakiepushwa kutumia vinywaji vyenye sukari. Ni muhimu umpe kiasi hicho cha maji siku zote bila kujali majira ya mwaka, hata hivyo mahitaji ya maji huongezeka zaidi wakati wa mazoezi, homa ya kuharisha n.k.
Umri wa mtoto na kiasi cha maji anayotakiwa kunywa kwa siku
Kikombe kimoja cha chai katika makala hii imetumika kumaanisha ujazo sawa na robo lita ya maji, yaani mililita 250 za maji. Baadhi ya bilauri au vikombe vya maji huwa na mililita 200 hadi 250. Ili kufahamu kiasi unachompa mwanao, nunua glasi yenye namba za vipimo vinavyoonyesha kiasi cha maji kwa mililita, au pima tafuta kikombe au bilauri yenye uwezo wa kuweka mililita 250 za maji iwe ndo kipimo chako.
Kumbuka
Mahitaji ya maji huongezeka kwenye mazingira ya joto, kufanya mazoezi, kuugua magonjwa ya kuharisha n.k.
Watoto chini ya miezi sita wanapata kiwango cha maji ya kutosha kwa kunyonya maziwa ya mama, hivyo unashauriwa usimnyweshe maji isipokuwa endapo umeshauriwa na daktari wako.
Endapo mtoto ana magonjwa ya moyo au mengine ambayo yanasababisha asitumie maji kwa wingi, unashauriwa usimpatie maji kwa wingi mpaka utakapo wasiliana na daktari wako kwa ushauri zaidi.
Mtoto chini ya miaka 4
Kiasi cha maji anapaswa kunywa ni vikombe viwili (2) hadi vi nne (4) kila siku
Mtoto wa miaka 4 hadi 8
Kiasi cha maji anapaswa kunywa ni vikombe vitano (5) kila siku
Mtoto wa miaka 9 hadi 13
Kiasi cha maji anapaswa kunywa ni vikombe saba (7) hadi nane (8) kila siku
Mtoto wa miaka 14 na zaidi
Kiasi cha maji anapaswa kunywa vikombe nane (8) hadi kumi na moja (11) kila siku
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
