Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Salome A, MD
24 Agosti 2026, 03:43:15

Kunyonyesha huku umekunja nne huweza kukufikasha kileleni
Inafahamika kisayansi kuwa, baadhi ya wanawake wanaonyonyesha , mtoto anaponyonya chuchu huamsha hisia kali za kingono zinazoweza kupelekea mama kufika kileleni wakati wa kunyonyesha huku amekunja nne. Hii ni kawaida kifiziolojia, mama anashauriwa kuacha kukunja nne wakati wa kunyonyesha endapo kupatwa na hisia hii inamfanya ajihukumu.
Hata hivyo baadhi ya wamama hujihukumu sana wanapopata hisia hizi, isitoshe wengine huamua acha kunyonyesha kabisa kuhofia kupata hisia hizo zinazoamshwa na mtoto anayenyonya. Baadhi ya wamama wanaporipoti hali hii kwa watu wasio wataalamu wa afya au wataalamu wa afya, watu hawa hushangaswa , humchukuliwa mama mkosaji na hata kumtilia shaka mama kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mtoto.
Kwanini mama anapata hisia za ngono na anafika kileleni ankinyonyesha huku amekunja nne?
Tafiti zinaonyesha kuwa, hali hii ya kufika kileleni inaweza kuashwa kwa kiasi kikubwa endapo mama atakunja nne wakati wa kunyonyesha. Hii ni kwa sababu, mama anapokunja nne, hukutanisha mashavu madogo ya uke na kufanya yasuguane na kusugua kinembe na kisha kufanya mama apate mshindo mkubwa kutokana na kugusana kwa kinembe na mashavu madogo pamoja na madhara ya homoni oxytocin inayosababisha ongezeko la mshindo.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
