Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Helen L, M.D
2 Aprili 2026, 16:17:51

Kupunguza uzito, kunywa maji kabla ya kula
Kunywa nusu lita ya maji ya uvuguvugu dakika 30 kabla ya mlo wowote ule, ikifuatiwa na kula chakula chenye nishati kidogo. Tabia hii huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza uzito mkubwa kupita kiasi.
Kwanini maji ya uvuguvugu
Tafiti zinaonyesha kuwa, kunywa nusu lita ya maji ya uvuguvugu nusu saa kabla ya kula hupelekea kusababisha hisia za kushiba na ongezeko la umeng'enyaji wa chakula. Matumizi ya maji kabla ya kula kwa ujumla hupelekea kula chakula kwa kaisi kidogo.
Matokeo mazuri ya kupungua uzito hutokea endapo matumizi ya maji ya uvuguvugu yatafuatiwa na utumiaji wa chakula chenye nishati kidogo.
Njia hii ni znuri kwa umri gani?
Njia hii imeonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza uzito kwa watu wenye umri wa kati na wazee, wenye uzito mkubwa kupitiliza. Hata hivyo njia hii inaweza kutumika kwa vijana wadogo pia walio na uzito mkubwa kupitiliza lakini ufanisi wake si mkubwa kama kwa watuw enye umri wa kati na wazee.
Je kuna madhara ya kutumia maji ya uvuguvugu kabla ya kula?
Tafiti zinaonyesha ni nadra sana watumiaji kupata madhara kwa kutumia kiasi hiki cha maji kabla ya kula. Matumizi ya maji ya baridi huonekana kupunguza uwezo wa mwili kumeng'enya chakula na kuongeza matatizo ya mfumo wa tumbo
Kina nani hawapaswi kutumia njia hii?
Baadhi ya watu wenye matatizo figo au moyo ulioferi, hawapaswi kutumia njia hii. Endapo pia umeshauriwa kutotumia njia hii kutokana na afya yako, usitumie njia hii pia mpaka pale utakapo shauriwa na daktari wako.
Vyakula gani vina nishati kidogo?
Mfano wa vyakula vyenye nishati kidogo vimeorodheshwa hapa chini, kuhusu matumizi ya vyakula hivyo soma kwenye makala zingine ndani ya tovuti hii.
Baadhi ya vyakula vyenye nishati kidogo ni;
Vyakula vya nafaka zisizokobolewa kama mahindi, mtama, uwele
Chakula chochote chenye mboga za majani kwa wingi
Matunda kama tikiti maji, parachichi, tufaa
Maboga
Mayai
Nyama isiyo na mafuta
Samaki
Mbegu za chia
Maziwa mgando
Vyakula hivi vyote vikitumiwa kwa kaisi kikubwa zaidi ya kawaida vitakupa nishati nyingi, unashauriwa kutumia kwa kiasi kinachoshauriwa kiafya.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
