Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Benjamin L, MD
Dkt. Adolf S, MD
2 Aprili 2026, 16:17:51

Kutolewa ovari mwanzoni mwa ujauzito
Mara baada ya uchavushaji kutokea na ujauzito kutambulika kwenye vipimo, kopas lutea , kovu linalobakia kwenye ovari baada ya kupasuka kutoa yali lilichavushwa kutengeneza kijusi huendelea kuzalisha homoni progesterone inayofanya ujauzito uendelee.
Kiwango cha homoni progesterone hufikia kilele siku ya 20 tangu kuchavushwa na kisha hupungua taratibu kwenda kwenye kiwango cha kawaida mpaka siku ya 40 hadi 45. Wakati wa kupungua huku, kopasi lutea za upili ambazo huamshwa na homoni chochezi ya foliko (FSH) huanza kuzalisha homoni progesterone na hivyo kupelekea ongezeko la homoni hii kuendelea kwenye damu ili kuhakikisha kuwa ujauzito unaendelea.
Kufanyiwa upasuaji wa kuondoa ovari zote kabla ya siku ya 60 ya ujauzito lakini si zaidi ya siku 80 hupelekea mimba kutoka na kichanga kufyonzwa.
Baada ya siku 60 kupita, ujauzito hutunzwa kwa homoni progestin (homoni inayofanana na progesterone) inayozalishwa na kondo la nyuma kuanzia siku ya 60 hadi 80. Kiango cha homoni hii huonezeka kwenye damu mpaka wakati wa kujifungua.
Nini unatakiwa kufahamu zaidi?
Mara baada ya kutolewa ovari, kichanga kwenye mji wa mimba anaweza kutoka kama hhedhi au kwa kufyonzwa na mwili wa mama.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
