Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Charles W, M.D
2 Aprili 2026, 16:17:51

Magonjwa 10 yanayoongoza kuua watu Tanzania
Magonjwa 10 yanayoongoza kuua watoto na watu wazima Tanzania ni Malaria, Magonjwa ya mfumo wa chini wa upumuaji, UKIMWI, Upungufu wa damu, Magonjwa ya moyo na misipa ya damu, Majeraha, Saratani, Kusambaa kwa sumu ya bakteria kwenye damu, Madhaifu ya kiuumbaji na Kiharusi. Chukua tahadhari, fahamu kuhusu magonjwa hayo, jifunze na jikinge endapo inawezekana.
Kutokana na tafiti ya afya kuangalia magonjwa yanayoongoza kuua watu kwenye hospitali za Tanzania, tafiti ya kuanzia mwaka 2006 hadi 2015 yenye jina la ‘Cause-specific mortality patterns among hospital deaths in Tanzania, 2006-2015’ ilofanywa na Leonard E. G. Mboera na wengine inaonyesha taarifa zinazofuata hapa chini
Magonjwa 10 yanayoongoza kuua watoto na watu wazima Tanzania
Malaria
Magonjwa ya mfumo wa upumuaji wa chini
Ukimwi HIV/AIDS
Upungufu wa damu
Magonjwa ya moyo na misipa ya damu
Ajali
Saratani
Kusambaa kwa sumu ya bakteria kwenye damu
Madhaifu ya kiuumbaji
Kiharusi
Magonjwa 10 yanayoongoza kuua watu wazima Tanzania
Malaria
HIV/AIDS
Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu
Magonjwa ya mfumo wa upumuaji
Saratani
Upungufu wa damu
Majeraha
Kiharusi
Kifua kikuu
Kusambaa kwa sumu ya bakteria kwenye damu
Magonjwa 10 yanayoongoza kuua watoto Tanzania
Malaria
Magonjwa ya mfumo wa upumuaji
Magonjwa ya madhaifu ya watoto
Upungufu wa damu
Magonjwa kutokana na kujifungua kabla ya wakato
Kusambaa kwa sumu ya bakteria kwenye damu
Madhaifu ya upumuaji kutokana na kuzaliwa kabla ya mapafu kukomaa
Matatizo wakati wa kujifungua
Utapiamlo
Matatizo ya mama au mtoto wakati wa ujauzito
Kumbuka
Baadhi ya magonjwa yanayoongoza kuua watu yanaweza kuzuilika. ULY CLINIC Inakushauri upende kufahamu kuhusu magonjwa hayo na namna ya kuchukua hatua za kujikinga. Soma zaidi kuhusu magonjwa hayo kwenye makala zilizopo ndani ya tovuti hii.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
