Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Mangwella S, mD
Dkt. Benjamin L, MD
2 Aprili 2026, 16:07:19

Majira na dawa za kifafa
Hapana!
Unashauriwa kutotumia dawa ya majira kama una kifafa au unatumia dawa za kifafa.
Dawa za kifafa ambazo hazipaswi kutumika pamoja na dawa za uzazi wa mpango ni pamoja na;
Dawa kundi la barbiturates
Carbamazepine
Oxcarbazepine
Phenytoin
Primidone
Topiramate
Kwanini usitumie dawa hizi na majira ya vichocheo viwili?
Dawa za kutibu kifafa zikitumika pamoja na majira yenye vichocheo viwili hufanya majira yenye vichocheo viwili kushindwa kufanya kazi yake.
Njia gani unapaswa kuchagua?
Kama unatumia dawa za kifafa na unataka kutumia njia ya uzazi wa mpango, tumia njia isiyo na kichocheo cya projestini au kipandikizi.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:07:19
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
