top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dr.Sospeter Mangwella, MD

24 Agosti 2026, 03:43:15

Malengelenge makubwa

Tatizo la malengelenge makubwa ni hali ya ngozi inayojitokeza kwa uvimbe mkubwa juu ya ngozi uliosheheni maji. Jeraha hili hujulikana pia kam bulla, na huwa na kipenyo kinachozidi milimita 5 (cm 0.5). Hali hii hutokea juu ya ngozi (epidermis) au chini yake, na huweza kuwa sehemu ya dalili ya magonjwa mbalimbali ya ngozi.


Sifa za malengelenge makubwa

  • Huwepo kama uvimbe mkubwa, wa duara au wa umbo la yai, wenye maji wazi, ya njano au yenye damu.

  • Unaweza kuwa laini au mgumu kutegemea chanzo.

  • Ukipasuka, huacha jeraha wazi linaloweza kuambukizwa kirahisi.

  • Hutokea popote mwilini – hususani miguu, mikono, usoni au sehemu za msuguano.


Visababishi vya malengelenge makubwa


a) Magonjwa ya kiautoimmuni
  • Pemphigus vulgaris – kinga ya mwili hushambulia ngozi.

  • Bullous pemphigoid – mara nyingi huathiri wazee.

  • Dermatitis herpetiformis – huhusiana na aleji ya gluteni.


b) Maambukizi
  • Herpes zoster – malengelenge hufuata neva moja.

  • Impetigo bullosa – husababishwa na bakteria, mara nyingi kwa watoto.


c) Mzio na Msuguano
  • Mzio wa mguso– mwitikio dhidi ya kemikali, mimea, vipodozi.

  • Malenge msuguano – msuguano mkali (kwa mfano viatu vipya).


d) Athari za Dawa
  • Sindromu ya Stevens-Johnson (SJS)

  • Neckrosisi ya usumu kwenye epidemis (TEN)


Uchunguzi wa kliniki

  • Historia ya ugonjwa (lini lilianza, eneo lililoathirika, dawa alizotumia).

  • Uchunguzi wa maabara: biopsy ya ngozi, immunofluorescence.

  • Kupima maji yaliyomo ndani ya jeraha iwapo yamepasuka.


Tiba na utunzaji

  • Tiba hutegemea chanzo:

    • Dawa za kupunguza kinga kali ya mwili kwa magonjwa ya autoimmune.

    • Antibiotiki iwapo kuna maambukizi ya bakteria.

    • Steroid (ya kupaka au ya kunywa).

  • Usafi wa jeraha na matibabu ya lishe ni muhimu kuzuia uambukizo.

  • Usipasue lengelenge bila ushauri wa daktari.


Tahadhari

  • Malengelenge makubwa ni dalili si ugonjwa mmoja, hivyo usijitibu bila uchunguzi wa daktari.

  • Mara nyingine, hali hii huashiria ugonjwa mkubwa unaohitaji matibabu ya haraka.


Rejea za mada hii
  1. Schmidt E, Zillikens D. Pemphigoid diseases. Lancet. 2013;381(9863):320–32. doi:10.1016/S0140-6736(12)61140-4.

  2. Bolognia JL, Schaffer JV, Cerroni L. Dermatology. 4th ed. Elsevier; 2017. p. 253–266.

  3. Wolverton SE. Comprehensive Dermatologic Drug Therapy. 3rd ed. Elsevier; 2013. p. 350–359.

  4. Siroy A, Wasman J, Tyler W. Clinical presentation of bullous skin disorders. Am Fam Physician. 2011;84(5):591–598.

  5. Hertl M, et al. Diseases of autoimmunity affecting the skin. Nat Rev Rheumatol. 2020;16(6):362–76. doi:10.1038/s41584-020-0403-2.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:07:37

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

bottom of page