Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
2 Aprili 2026, 19:17:51

Matumizi sahihi ya dawa
Matumizi sahihi ya dawa hujumuisha mgonjwa kupokea dawa sahihi kulingana na mahitaji yake ya kiafya, katika dozi sahihi, muda sahihi wa matibabu na kwa bei anayoweza kumudu. Epuka madhara na gharama kwa kuzingatia matumizi sahihi ya dawa.
Matumizi sahihi ya Dawa ni nini?
Ili matibabu yafanikiwe, ni lazima mtoa dawa na mtumiaji waweze kupeana maelekezo sahihi ya matumizi ya dawa. Kutumia dawa sahihi kwa usahihi, hupunguza madhara ya dawa na gharama kwa mgonjwa.
Matumizi sahihi ya dawa hujumuisha mgonjwa kupokea dawa sahihi kulingana na mahitaji yake ya kiafya, katika dozi sahihi, muda sahihi wa matibabu na kwa bei anayoweza kumudu. Ishara za matumizi sahihi ya dawa ni;
Kutumia dozi sahihi
Kumaliza kozi
Kutumia dawa sahihi katika kutibu ugonjwa
Kutumia dawa kwa njia sahihi
Kununua na kutumia dawa baada tu ya kufanyiwa uchunguzi
Kutumia dawa yenye kiwango cha ubora
Kutumia dawa zisizoingiliana kiutendaji
Kutumia viuajisumu( antibayotiki) kutibu magonjwa yanayotokana na bakteria
Kutumia dawa za viuajivirusi kutibu magonjwa yanayotokana na virusi
Kutumia dawa bila pombe au vyakula vyenye muingiliano na dawa
Kutumia dawa zinazoruhusiwa wakati wa ujauzito
Sababu zinazochangia matumizi yasiyo sahihi ya dawa
Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuchangia matumizi sahihi ya dawa ambazo ni;
Kugundua ugonjwa
Uandikaji sahihi wa dawa
Utoaji sahihi wa dawa
Kumudu gharama za dawa
Mgonjwa kutumia dawa kwa usahihi
Mgonjwa kutumia dawa baada ya kupata ushauri wa daktari
Faida za matumizi sahihi ya dawa
Kuboresha afya ya mtumiaji wa dawa
Kutimiza Lengo sahihi la matumizi ya dawa husika
Kupunguza uwezekano wa kujenga usugu wa vimelea vya magonjwa
Kupunguza madhara/Maudhi ya dawa
Kupunguza gharama zisizo za lazima kwa mgonjwa na Serikali
Kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa yatokanayo na utumiaji sugu wa dawa
Jamii kuwa na Imani na dawa pamoja na mifumo ya kutolea huduma za afya
Athari zitokanazo na matumizi yasiyo sahihi ya dawa
Mgonjwa asipotumia dawa kwa usahihi yafuatayo yanaweza kutokea;
Mgonjwa hatapata tiba sahihi na hivyo kuendelea kuugua au kufa
Uwezekano wa kupata madhara ya dawa
Wajibu wa Mtoa Dawa na mgonjwa katika kuchangia matumizi sahihi ya dawa
Ili kuhakikisha dawa zinatumika kwa usahihi, Mtoa Dawa na mgonjwa wanapaswa;
Kugundua kwa usahihi dalili za ugonjwa na kufanya uchunguzi kabla ya kutumia dawa
Kutoa rufaa kwa mgonjwa kwenda ngazi inayohusika kulingana na mahitaji ya kiafya
Kumpa na kutumia dawa sahihi kulingana na cheti cha daktari au maelezo ya mgonjwa (dawa inatakiwa kuandikwa na daktari kabla ya kutumia)
Kutoa na kupokea maelekezo juu ya matumizi na uhifadhi sahihi wa dawa.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
