Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Mangwella S, MD
Dkt. Benjamin L, MD
24 Agosti 2026, 03:43:22

Maumivu ya fantomu
Fantomu ni hisia ya maumivu kutoka kwenye kiungo cha mkono au mguu kilichotengwa na mwili kwa upasuaji baada ya kuharibiwa na ugonjwa au ajali. Hutokea sana kwa wagonjwa waliokuwa na maumivu makali kabla ya upasuaji, tiba yake hutofautiana baina ya mtu na mtu na huhusisha matumizi ya dawa mbalimbali kabla ya kufahamu ipi inayofaa zaidi.
Historia ya maumivu ya Fantamu
Hapo zamani ilifahamika kuwa maumivu ya fantomu yanahusiana na matatizo ya kisaikolojia yanayotokea kwa wagonjwa baada ya kukatwa kiungo cha mwili kutokana na maumivu makali hata hivyo wanasayansi kwa sasa wanafahamu kuwa maumivu haya huanzia kwenye mfumo wa kati wa fahamu. Maumivu ya fantomu hufahamika kwa majina mengine ya;
'Mguu wa fantamu'
'Mkono wa fantomu'
'Maumivu makali baada ya kukatwa mkono',
'Maumivu makali baada ya kukatwa mguu'
Na kwa lugha ya kiingereza hufahamika kama;
'phantom pain'
'phantom limb;'
Vihatarishi
Si kila mtu atapata maumivu ya fantomu baada ya kuondolewa kiungo cha mwili, baadhi ya watu wenye vihatarishi vifuatavyo huwa na uwezekano mkubwa wa kupata maumivu haya;
Kuwa na maumivu kabla ya kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa kiungo cha mwili. Hii inaweza kutokana na ubongo kutofuta kumbukumbu za kiungo cha mwili na hivyo kuendelea kutuma ishara za maumivu hata baada ya kiungo kuondolewa.
Maumivu ya sehemu ya kiungo kilichobaki baada ya upasuaji. Watu wenye maumivu ya kiungo kilichobaki baada ya upasuaji mara nyingi hupata maumivu ya fantomu. Maumivu ya kiungo kilichobaki huwza tokana na majeraha yaliyotokea kwenye mshipa wa fahamu wakati wa kukata kiungo au kukua vibaya kwa mshipa wa fahamu.
Dalili
Mbali na maumivu, sifa za maumivu ya fantomu ni;
Huanza ndani ya wiki la kuondolewa kiungo cha mwili hata hivyo yanaweza kutokea baada ya mwezi toka kufanyiwa upasuaji
Maumivu huja na kutoka
Maumivu huathiri sehemu ya mguu iliyo mbali na kiungo cha mwili mfano kanyagio ambalo limetolewa
Maumivu huelezewa kama ya kuchoma mithiri yam shale, kubana, kuchoma kama sindanol kuchanachana na kuungua
Matibabu
Ingawa hakuna dawa maalumu kwa kila mtu kwa ajili ya maumivu ya fantomu, dawa zinazotumika katika matibabu ya maumivu mbalimbali zinaweza kumsaidia mgonjwa. Hata hivyo dawa hizi huwa hazina ufanisi kwa kila mtu yaani kila mtu anaweza kunufaika na dawa ambayo haijamsaidia mwingine. Dawa zinazotumika kwenye matibabu ya maumivu ya fantomu ni pamoja na;
Dawa za maumivu mfano . Acetaminophen, ibuprofen, naproxen sodium
Dawa za jamii ya Antidepressants mfano amitriptyline, nortriptyline, tramadol
Dawa za kutibu degedege mfano; gabapentin, Neurontin, pregabalin
Dawa jamii ya Narcotiki mfano. codeine na morphine
Dawa jamii ya N-methyl-d-aspartate (NMDA) risepta agnonisti mfano dextromethorphan
Kinga ya maumivu ya fantomu
Kutokana na kuwa na hatari kubwa ya kupata maumivu ya fantomu kwa wagonjwa waliokuwana na maumivu kabla ya kukatwa kiungo cha mwili, Daktari atachukua hatua ya kukupa ganzi ya nusu kaputi masaa au siku chache kabla ya kufanyiwa upasuaji. Hii itapunguza maumivu haraka baada ya upasuaji na kuondoa hatari ya kupata maumivu ya muda mrefu ya fantomu.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
