Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. peter A, MD
2 Aprili 2026, 16:07:13

Mimba baada ya kuacha majira
Wanawake ambao wameacha kumeza Vidonge vya majira yenye vichocheo viwili wanaweza kupata mimba haraka kama ilivyo wanawake walioacha kutumia njia nyingine za uzazi wa mpango zenye vichocheo.
Vidonge vya majira yenye vichocheo viwili havicheleweshi kurejea kwa uwezo wa mwanamke kutunga mimba baada ya kuacha kuvimeza. Mpangilio wa hedhi uliokuwa nao kabla hajatumia majira yenye vichocheo viwili kwa kawaida hurudi baada ya kuacha kuvimeza.
Je, tafiti zinasemaje kuhusu muda wakunasa mimba?
Tafiti zilizofanyika zinaonyesha kuwa asilimia takribani 80 ya wanawake walioacha kutumia njia za uzazi wa mpango ikiwa na vidonge vya majira yenye vichocheo viwili, hupata mimba ndani ya miezi 12. (Tadele Girum, et al)
Inaweza chukua mmuda mrefu kurejea kwa hedhi?
Ndio! baadhi ya wanawake inawabidi kusubiri miezi michache kabla ya mpangilio wao wa kawaida wa hedhi kurejea.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:07:13
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
