Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
24 Agosti 2026, 03:43:15

Muda sahihi kusoma kipimo cha HIV SD bioline
HIV 1/2 SD BIOLINE 3.0 ni kipimo cha haraka chenye uwezo wa kutambua uwepo wa antibodi zilizozalishwa na mfumo wa kinga ya mwili kupambana na maambukizi ya kirusi HIV1 au HIV2. Majibu ya kipimo ni sahihi kama yatasomwa ndani ya dakika 10 hadi 20, majibu baada ya muda huu si ya kuaminika.
Kipimo cha HIV SD bioline
Swali
Ukipima VVU kwa kwa kipimio cha HIV SD bioline na kikachora mstari mmoja kwenye C kisha baada ya masaa matatu ikachora mistari wa pili yaani mstari kwenye alama C na 1 au 2 na baada ya hapo akatumia kipimo cha unigold ikasoma mstari mmoja zaidi ya mwaka ikawa hivyo je mtu huyo ni mgonjwa au?
Jibu ni Hapana
HIV 1/2 SD BIOLINE 3.0 ni kipimo cha haraka chenye uwezo wa kutambua uwepo wa antibodi IgG, IgM na IgA zilizozalishwa na mfumo wa kinga ya mwili kupambana na maambukizi ya kirusi HIV1 au HIV2. Majibu ya kipimo yatakuwa sahihi kama yatasomwa ndani ya dakika 10 hadi 20 kabla ya kutupa kipimo hicho sehemu salama kama ulivyoshauriwa na daktari wako.
Namna kilivyotengenezwa
Kipimo cha SD BIOLINE HIV-1/2 kimewekewa utando wa antijeni za kirusi cha HIV1 (glaikoprotini gp 41 na protini 21) kwenye mstari namba 1 na antijeni za kirusi cha HIV2 (glaikoprotini 36)kwenye mstari namba 2. Sampuli ya damu inapowekwa huanza kutembea kutoka kwenye kitundu cha sampuli kwenda kwenye mstari namba moja, mbili na mwisho kwenye mtari wenye alama C. Mstari C hutumika kuangalia kama kipimo kinafanya kazi, mstari huu utaonekana mara utakapoweka sampuli ya damu au ukaweka kizimulio cha sampuli (maji ya kipimo)
Mistari yote mitatu inatakiwa isionekane kabla ya kuweka sampuli au maji ya kuzimulia sampuli.
Wakati gani wa kusoma majibu
Majibu yanapaswa kusomwa ndani ya dakika 10 hadi 20. Baada ya kuongeza kizimulio, soma majibu yako baada ya dakika 10 lakini si zaidi ya dakika 20.
Kwa majibu chanya ya HIV (Positive), lazima mistari miwili ionekane, mmoja wapo ukiwa kwenye C na mwingine kwenye HIV1 au HIV2.
Ufanye nini kama majibu hayaonekani vema baada ya dakika 10?
Kama majibu hayasomeki vema baada ya dakika kumi kwa sababu ya rangi nyekundu kutawala, soma upya baada ya dakika 10 lakini isiwe zaidi ya dakika 20 toka umeongeza kizimulio.
Je kwanini kipimo kinasoma mistari mitatu?
Ni kwa nadra sana kwa binadamu kupata maambukizi ya HIV1 na d HIV2 kwa pamoja. Kuonekana kwa mstari wa HIV1 na HIV2 mara nyingi humaanisha mwitikio wa kipimo kwenye protini zinazoelekea kufanana kati ya HIV1 na HIV 2. Ili kuthibitisha kwamba mtu ana virusi vya aina zote mbili, vipimo zaifi vya uthibitisho vinatakiwa fanyika.
Kama majibu yakisoma mistari miwili au zaidi ufanyenini kupata majibu ya mwsisho?
Mara nyingi kipimo cha SD bioline kinaposoma mistari miwili au zaidi ambapo kati ya mistari hiyo lazima Mstari C uwepo ina maanisha kuwa mtu huyu ana uwezekano wa kuwa na maambukizi ya VVU au magonjwa mengine kama kaswende, lupus na ugonjwa wa lyme.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
