Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Helen L, M.D
2 Aprili 2026, 16:17:50

Muda unaotosha kulala
Muda wa kulala kiafya hutegemea umri wa mtu na hupungua kwa jinsi umri unavyoongezeka. Mfano kichanga anapaswa kulala angalau muda wa masaa 14 hadi 17, vijana wadogo, masaa 7 hadi 9, wazee wa miaka 65 na zaidi, ni masaa 7 hadi 8 wakati wa usiku. Lala muda wa kutosha kwa afya yako
Muda wa kulala kulingana na umri
Kwa vinaja wadogo na watu wazima, wanashauriwa kulala kulala angalau kwa muda wa masaa 8 hadi 9 mfululizo wakati wa usiku, wakati huo watoto wadogo wanatakiwa kulala masaa mengi zaidi kuliko watu wazima au wazee. Ukilala muda wa kutosha utaimarisha mwili wako kiakili na kifizikia, watoto wadogo pia wanapaswa kulala muda wa kutosha ili wakue vema. Usiwe na tabia ya kulala muda pungufu au zaidi ya masaa yanayoshauriwa kiafya.
Umri wa siku 0 hadi miezi 11
Watoto wenye siku 0 hadi umri wa miezi 3
Muda wa kulala ni angalau masaa 14 hadi 17 kwa siku
Watoto wenye umri wa miezi 4 hadi miezi 11
Muda wa kulala ni angalau masaa 12 hadi 15 kwa siku
Umri wa Mwaka 1 hadi miaka 5
Watoto wenye umri wa mwaka 1 hadi miaka 2
Muda wa kulala ni angalau masaa 11 hadi 14 kwa siku
Watoto wenye umri wa miaka 3 hadi miaka 5
Muda wa kulala ni angalau masaa 10 hadi 13 kwa siku
Umri wa miaka 6 hadi 17
Watoto wenye umri wa miaka 6 hadi miaka 13
Muda wa kulala ni angalau masaa 9 hadi 11 mfululizo kwa siku
Watoto wenye umri wa miaka 14 hadi miaka 17
Muda wa kulala ni angalau masaa 8 hadi 10 mfululizo kwa siku
Umri wa miaka 18 na zaidi
Vijana wadogo wenye umri wa miaka 18 hadi miaka 25
Muda wa kulala ni angalau masaa 7 hadi 9 mfululizo kwa siku
Watu wazima wenye umri wa miaka 26 hadi miaka 64
Muda wa kulala ni angalau masaa 7 hadi 9 mfululizo kwa siku
Wazee wenye umri wa miaka 65 au zaidi
Muda wa kulala ni angalau masaa 7 hadi 8 mfululizo kwa siku
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:17:50
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
