top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

Dkt. Helen L, M.D

24 Agosti 2026, 03:43:22

Osha na chemsha mayai kujikinga na Taifod

Viumbe jamii ya ndege wenye maambukizi ya kimelea cha ‘salmonella’ kinachosababisha taifodi, huzalisha mayai yenye vimelea hao. Hata hivyo pia yai huweza kubeba vimelea kwa nje endapo litagusa kinyesi chenye vimelea. Osha na chemsha mayai yako kuepuka maambukizi hayo


Viumbe jamii ya ndege kama kuku, bata n.k wenye maambukizi ya taifod, huweza kuzalisha mayai yenye vimelea hao. Vimelea vya maradhi huingia kwenye mayai wakati wa kutengenezwa, kabla ya yai kupata ganda lake gumu. Hata hivyo pia mayai endapo yatakutana na kinyesi cha ndege chenye maambukizi, vimelea hao hubakia kwenye magamba ya yai. Endapo utatumia mayai haya bila kuzingatia kanuni za kiafya, utapata maambukizi hayo.


Namna ya kuandaa mayai ili kuepuka maabukizi ya taifod


  • Chemsha yai lako mpaka liwe gumu kwa ndani au pasua na kukaanga liive mpaka kupata rangi ya kahawia

  • Kama unataka kutengeneza chakula cha mayai mabichi, tumia mayai yaliyotakaswa kwa kuondolewa vimelea vya maradhi

  • Kula au weka kwenye jokofu chakula chako mara moja baada ya kupika.

  • Nawa mikono na safisha vyomba ambavyo vimegusa mayai mabichi ikiwa pamoja na sufuria, sahani n.k

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:17:51

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

1.Salmonella and Eggs. https://www.cdc.gov/foodsafety/communication/salmonella-and-eggs.html. Imechukuliwa 07.02.2021 2.FDA. What You Need to Know About Egg Safety. https://www.fda.gov/food/buy-store-serve-safe-food/what-you-need-know-about-egg-safety. Imechukuliwa 07.02.2021 3.Egg Products and Food Safety. https://www.fsis.usda.gov/wps/portal/fsis/topics/food-safety-education/get-answers/food-safety-fact-sheets/egg-products-preparation/egg-products-and-food-safety/CT_Index. Imechukuliwa 07.02.2021
bottom of page