Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Lugoda B, MD
Dkt. Adolf S, MD
2 Aprili 2026, 16:17:51

Tiba takatifu ya kiharusi mpito
Kiharusi ni upotevu wa kazi za kiselebramu unaodumu kwa masaa 24 unaodhaniwa kusababishwa na ukosefu wa damu kwenye sehemu hiyo ya ubongo iliyoathirika au mvio wa damu kwenye tishu za ubongo (haswa kutokana na kupasuka kwa mishipa ya ubongo)
Wagonjwa wa kiharusi cha mpito wakiwa hospitali mara nyingi hupatiwa tiba inayolenga kudhibiti dalili na kuzuia kutokea kwake kwa mara nyingine. Mara baada ya kufanyika kwa vipimo na matibabu mgonjwa huruhusiwa kwenda nyumbani na kupangiwa tarehe ya kuhudhuria kliniki ili kufuatiliwa maendeleo yake kw akufanyiwa vipimo tena na kupewa dawa.
Wataaalamu wa afya husahau vipengele muhimu katika matibabu takatifu ya kiharusi cha mpito ambacho ni elimu ya kutosha kwa mgonjwa husika na katika lugha yake rahisi.
Kipengele hiki ni muhimu kwa kuwa kuna mambo mengi yanayotokea katika maisha ya mgonjwa baada ya kupata matibabu ya awali ambayo yakipewa kipaumbele husaidia katika kutoa matibabu takatifu. Makala hii imeorodhesha mambo hayo. Maelezo zaidi yanapatika kwa kubofya makala husika.
Mabakia ya kiharusi mpito
Mara baada ya mgonjwa kupata kiharusi cha mpito au kiharusi kidogo, kuna athari zinazobakia kwa mgonjwa ambazo zimeitwa katika makala hii kama “mabakia ya kiharusi mpito”. Mabakia ya kiharusi mpito yanaweza kutokea wakati wowote baada ya mgonjwa kupata kiharusi. Baadhi ya mabakia ya kiharusi cha mpito au kiharusi kidogo yanayopaswa kupewa kipaumbele ili kutoa matibabu takatifu ya kiharusi yanayopaswa kufahamika na mgonjwa pamoja na wataalamu wa afya ni pamoja na:
Athari za kihisia na hali ya moyo
Athari za utendaji wa akili
Uchovu mkali
Udhaifu wa mwili
Udhaifu wa uono
Udhaifu wa maongezi
Kila athari imeelezewa sehemu nyingine katika tovuti hii.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
