Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
2 Aprili 2026, 16:17:51

Umri mzuri wa kushika mimba
Mwanamke anapozaliwa huwa na mayai takribani milioni 2 yanayopungua kadri umri unavyoongezeka. Mayai elfu 25 husalia kwenye umri wa miaka 37 na elfu 1 kwenye umri wa miaka 51. Ili kushika ujauzito wenye matokeo mazuri kwako na mtoto, shika baada ya miaka 20 na kabla ya miaka 35.
Mahusiano ya ujauzito na umri
Kwa kawaida unaweza pata mimba mara unapoanza ona damu ya hedhi na kabla ya kuingia kipindi cha koma hedhi na wastani wa umri wa wanawake wengi kupata ujauzito huwa kati ya miaka 12 hadi 51.
Uwezo wa kushika mimba hupungua kwa jinsi unavyoongezeka umri kiasi cha kuwa vigumu sana kwenye umri kuanzia miaka 37 na kuendelea. Licha ya uwezo kupugnua, kupata mimba kwenye umri mkubwa zaidi huambatana na madhara mbalimbali kwa mama na mtoto.
Umri mzuri unaoshariwa kushika mimba yenye matokeo mazuri kwa mama na mtoto ni baaada ya miaka 20 na mwanzoni mwa miaka 30.
Je umri unadhuru vipi uwezo wa kubeba mimba?
Kwa kawaida mwanamke huzaliwa na mayai milioni 2 yanayo pungua idadi na ubora kadri umri unavyoongezeka. Mayai elfu 25 tu husalia unapofikisha umri wa miaka 37 na elfu 1 tu kwenye umri wa miaka 51. Uzazi hupungua kwa jinsi inadadi na ubora wa mayai unavyopungua
Mambo mengine yanayodhuru uwezo wa kubeba ujauzito kwenye umri mkubwa?
Kwa jinsi unavyoongezeka umri, hatari ya kupata matatizo mbalimbali ya uzazi kutokana na uzee na maambukizi huongezeka kiasi cha kuweza kusababisha usishike mimba kirahisi au kuwa na ujauzito wenye matokeo mabaya. Mfano wa magonjwa yanayodhuru ujauzito na hutokea ukubwani ni ugonjwa wa endometriosis na magonjwa ya mirija ya uzazi.
Mara unapofikisha umri wa miaka 32, uwezo wa kubeba mimba huanza pungua na unapoanza miaka 35 hadi 37, uwezo huo hupungua kwa kasi zaidi
Vihatarishi vinavyopunguza uwezo wa kushika mimba
Vihatarisi vingine vinavyopunguza uwezo wa kushika mimba ni;
Kuvuta sigra
Kutumia ya baadhi ya dawa za uzazi wa mpango
Matumizi ya baadhi ya dawa za kutibu saratani
Maambukizi kwenye via vya uzazi
Kuna hatari ya kubeba ujauzito kwenye umri mkubwa?
Kupata ujauzito baada ya miaka 35 huambatana na mambo yafuatayo;
Kisukari cha ujauzito
Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu
Kifafa cha mimba
Kujipandikiza kwa kondo karibu na njia ya uzazi
Ujauzito kutoka
Kujifungua njiti
Mtoto kufia tumboni
Kujifungua kwa upasuaji
Kutokwa na damu nyingi wakati wa ujauzito
Kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua
Kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo
Kujifungua mtoto mwenye sindromu ya down
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
