Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Helen L, M.D
2 Aprili 2026, 16:17:51

Usitupe chooni au kuchimbia aridhini dawa zilizoisha muda wa matumizi
Dawa zilizokwisha muda wake hupaswa kuteketezwa kwa utaratibu maalumu. Endapo umepewa maelekezo ya namna ya kuteketeza dawa zisizotumika, fuata maelekezo hayo kuziteketeza.Endapo hujapewa, zirejeshe kwa mfamasi au hospitali ili zikateketezwe kwa usalama. Usitupe chooni au kuchimbia aridhini, kuepuka madhara ya kiafya.
Kwanini usitupe chooni au kuchimbia aridhini?
Dawa zozote zile ikiwa pamoja na zile zilizokwisha muda wake, endapo zitachimbiwa aridhini au kutupwa chooni ni hatari kwani ni sumu kwenye mazingira pamoja na viumbe mbalimbali wanaoishi karibu au umbali wa mita kadhaa kutoka kwenye maeneo ya dawa hizo zilipoharibiwa. Endao dawa zitaharibiwa kwa njia hizi, madhara yake yanaweza kumpata binadamu kwa njia mbalimbali kama vile;
Kutumia viumbe au wadudu mbalimbali waliozaliwa katika maeneo uliyotupa dawa
Kula matunda au mboga zinazofyonza maji kutoka kwenyearidhi yenye dawa. Miti na mimea mingine inaweza kufyonza maji ya choo hata ikiwa ipo mita nyingi kutoka kwenye nyumba yako.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
