Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Sospeter B, MD
Dkt. Salome A, MD
2 Aprili 2026, 16:17:51

Utofauti wa HIV-1 na HIV-2
Kuna aina mbili za virusi vya UKIMWI vinavyofahamika, kirusi cha VVU1 ambacho kimesambaa duniani kote na kinasababisha UKIMWI kwa haraka na Kirusi cha HIV2 ambacho kipo Afrika magharibi ambacho hakina makali ya maambukizi.
Watu wengi duniani huwa na maambukizi ya kirusi cha HIV1. Wakati virusi vyote vinaharibu mfumo wa kinga ya mwili, kirusi cha HIV2 huharibu taratibu na kiwango cha kuambukiza huwa kidogo sana.
Mfanano wa HIV1 na HIV2
Kirusi cha HIV1 na HIV2 hufanana sifa ikiwa pamoja na:
Mpangilio sawa wa jeni
Namna inavyoambukizwa
Namna inavyojizalisha ndani ya seli
Madhara ya kirusi kwenye mwili
Utofauti wa HIV1 na 2
Licha ya HIV1 na 2 kufanana sana kama ilivyo hapo juu, kirusi cha HIV2 huwa nakasi ndogo ya maambukizi na uwezekano wake wa kusababisha UKIMWI huwa mdogo pia. Namna gani kuna utofauti wa kirusi cha HIV2 kusababisha UKIMWI bado haijafahamika vema.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
