Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Helen L, M.D
24 Agosti 2026, 03:43:22

Vyakula vyenye uwezo wa kukupa usingizi
Matumizi ya chai ya maua ya pasheni au chamomile, juisi ya tunda damu au kiwi, karanga ya lozi au jozi na nyama ya bata mzinga huchochea kupata usingizi kwa haraka. Endapo una tatizo la kukosa usingizi, tumia moja ya vitu hivyo.
Ni nini huamsha usingizi?
Usingizi huamshwa na homoni yenye jina la 'melatonin' inayozalishwa na tezi 'pineal' iliyopo ndani ya ubongo. Homoni hii hutolewa wakati wa usiku na huitwa kwa jina la 'homoni ya giza'. Kemikali na madini yanayoweza kukufanya uzinzie ni kama apigenin, magnesium na tryptophan. Matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye apigenin, magnesium, tryptophan na melatonin huchochea usingizi kutokana na kuwa au kuongeza uzalishaji wa homoni melatonin.
Vyakula vyenye Apigenin
Vyakula vyenye Apigenin kwa wingi ni kama;
Kotimiri (parsley)- tumia majani yake kutengeneza chai
Figili (celery)- tumia kama mboga
Chai ya Chamomile- tumia majani yake kutengeneza chai
Chai ya maua ya pasheni- tumia majani yake kutengeneza chai
Rubaruti (Artichokes)- tumia kama chakula
Vyakula vyenye tryptophan
Vyakula vyenye tryptophan kwa wingi ni kama;
Lozi (almond)- Tafuna angalau gramu 28
Nyama ya bata mzinga(turkey)- kula kama mlo wa usiku
Vyakula vyenye au vinavyosaidia kuzalisha Melatonin
Vyakula vyenye au vinavyosaidia kuzalisha Melatonin ni kama;
Matunda damu (tart chery)- tumia kama juisi angalau glasi moja au mbili kabla ya kulala
Mayai- tumia mayai mawili kabla ya kulala
Maziwa ya ng'ombe- kunywa angalau glasi moja kabla ya kupata usingizi
Mafuta au nyama ya samaki- tumia kama mlo au pikia chakula
Kiwi- tumia kama tunda au juisi isiyochujwa
Vyakula vyenye magnesium
Vyakula vyenye magnesium kwa wingi ni kama;
Lozi- tafuna angalau gramu 28 kabla ya kulala
Spinachi ya Vine/spinachi ya kawaida- tumia kama mboga ya majani
Mbegu za tikiti- tafuna angalau gramu 28 kabla ya kulala
Mbegu za boga- tafuna angalau gramu 28 kabla ya kulala
Korosho- tafuna angalau gramu 28 kabla ya kulala
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:50
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
