Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Peter A, MD
8 Novemba 2021
Chanjo za watoto
Chanjo za watoto hutolewa katika vipindi mbalimbali mtoto anapozaliwa.chanjo hizi hutolewa kwa malemgo ya kumkinga mtoto na magonjwa mbalimbali yanayoweza kutisia uhai Wa mtoto. Mzazi Wa mtoto, ni muhimu kumpeleka mwanao akapate chanjo Mara atakapozaliwa kwani utamkinga na maradhi yatayoweza kuleta ulemavu hata kifo
Aina gani ya chanjo hutolewa?
Chanjo ya donda koo, kifadulo,pepo punda (DPT)
chanjo ya TB au BCG
Change ya polio
Chanjo ya pneumococcal (PCV)
Chanjo ya rubella
Chanjo ya sulua
Chanjo ya rotavirus
Chanjo ya kirusi cha homa ya INI a in a B (hepatitis B)
Chanjo ya haemophilus influenza
Aina gani ya magonjwa yanaweza kuzuiwa na chanjo za watoto?
Magonjwa mbalimbali yanaweza kuzuiwa na chanjo hizi kama vile
Ugonjwa Wa surua - mtoto akipata chanjo ya surua
Ugonjwa Wa pepo punda kama mtoto akipata chanjo ya BCG
Polio(ugonjwa wa kupooza)-mtoto akipata chanjo ya polio
Ugonjwa Wa pneumonia ya pneumococcal kama mtoto akipata chanjo hiyo ya pneumococcal
Ugonjwa Wa kuhara unaosumbua sana na kuua watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja-chanjo ya rotavirus
Homa ya Ini kwa watoto
Wakati gani mtoto anatakiwa kupata chanjo?
Kila nchi inataratibu zake za kutoa chanjo hizi, ila Tanzania kwa utaratibu Wa EPI yaani expanded program of immunization inafuata utaratibu kama ufuatao;
Mtoto anapoozaliwa tu anatakiwa kupata chanjo ya BCG na polio 0 na hizi humkinga mtoto kupata pepopunda na
Mtoto anapofikisha wiki site yaani mwezi mmoja na wiki mbili anatakiwa kupoata chanjo ya polio1 na pentavalent1 kumkinga
Wiki 10 (miezi miwilki na wiki mbiki) anatakiwa kupata chanjo ya penta2 na polio2
Wiki 12 yaani miezi mitatu mtoto anatakiwa kupewa polio 3 na rotavirus
Mtoto akifkisha miezi Tisa anatakiwa kupelekwa hospitali kupata chanjo ya surua ili kujikinga na ugonjwa huo hatari
Elimu inayotolewa hapa ni kwa ajili ya ushauri tu na hivyo ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma makala hii.
Kwa ushauri zaidi na tiba, wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kupitia mawasiliano yetu
Imeboreshwa,
9 Novemba 2021 07:18:57
Rejea za mada hii:
CDC. Recommended Child and Adolescent Immunization Schedule for ages 18 years or younger, United States, 2021. https://www.cdc.gov/vaccines/schedules/hcp/imz/child-adolescent.html. Imechukuliwa 09.11.2021
IAC. Vaccinations for Infants and Children, Age 0–10 Years. https://www.immunize.org/catg.d/p4019.pdf. Imechukuliwa 09.11.2021