top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Peter A, MD

8 Novemba 2021

Hatua za ukuaji wa mtoto

Hatua zilizoelezewa hapa chini zimetokana na tafiti zilizofanywa na wanasayansi, hivyo zinatumika kama kipimo au rejea ya kusema mtoto wako ana maendeleo ya kawaida au yasiyo ya kawaida. Maendeleo ya mtoto yanapimwa kwenye vipengele vya mota, lugha

Mwezi 1 hadi 11

Ukuaji wa kimota

  • Mtoto mwenye mwezi mmoja anaweza kunyanyua kichwa kidogo anapokuwa kwenye pozi la kulala kifudifudi, pia anaweza kushika kitu mkinoni kwa nguvu endapo atapewa, mfano ukimwekea kidole atakishika kwa nguvu

  • Mtoto mwenye miezi mitatu hukaza shingo na anaweza kufungua mikono anapokuwa katulia, endapo utamnyanyua mtoto kutoka pozi la kulala utaona shingo yake haianguki kwa nyuma

  • Mtoto mwenye miezi minne hadi mitano anaweza kujigeuza anapokuwa amelala, anaweza kukaa kwa kuegemea vitu nyum yake bilakuanguka na anaweza kushika kitu kwa mikono miwili

  • Mtoto mwenye miezi sita anaweza kukaa vizuri bila kushikiliwa au kuwekewa kitu kwa nyuma, anaweza kuhamisha kitu kutoka mkono mmjoja kwenda mwingine pia kuchukua vitu kilicho pembeni

  • Mtoto mwenye miezi tisa anaweza kutambaa, kusimama kwa kushikilia vitu vilivyo pembeni yake, kunyanyua kitu kwa kutumia ncha za vidole, kujilisha kwa kutuma mikono yake

Mwezi 1 hadi 9


Mambo ya kijamii, ufahamu, hisia na lugha

  • Mtoto mwenye mwezi mmoja anaweza kushituka au kushangaa asikiapo sauti pia anaweza kutulia akiangalia sura ya mtu

  • Mtoto mwenye miezi mitatu huwa anatoa visauti, kufuata/kukubali vitu/watu anao wafahamu na anaweza kutabasamu

  • Mtoto mwenye miezi minne hadi mitano anatambua sauti pia anafurahia kuangalia mazingira

  • Mtoto mwenye miezi sita anaweza kutoa sauti za mikwaruzo/kuguna pia anatambua wageni

  • Mtoto mwenye miezi tisa anaanza kusema “dada/mama”, anaelewa akikatazwa kitu

Mwaka 1 hadi 5


Ukuaji wa kimota

  • Mtoto mwenye mwaka mmoja(miezi 12) anaweza kutembea mwenyewe, kurusha vitu

  • Mtoto mwenye miezi 15 anaweza kutembea kinyume, kupanda ngazi, kuchorachora

  • Mtoto mwenye miezi 18 anaweza kukimbia kujilisha kwa kutumia kijiko kubebanisha vitu vinne

  • Mtoto mwenye miezi 24 anaweza kupanda na kushuka ngazi, kuchuchumaa na kusimama, kijivua nguo na kubebanisha vitu vitano hadi sita

  • Mtoto mwenye miaka mitatu anaweza kuendesha baiskeli ya magurudumu matatu, kurusha mpira mikononi na anaweza kuchora duara

  • Mtoto mwenye miaka minne anaweza kushuka ngazi kwa kupishanisha miguu, kudaka mpira na kujivalisha nguo mwenyewe

  • Mtoto mwenye miaka mitano anaweza kufunga kamba za viatu mwenyewe

Mwaka 1 hadi 5


Ukuaji wa kijamii, ufahamu, hisia na lugha)

  • Mtoto mwenye miezi 12 anaweza kutamka neno moja hadi manane tofauti na “dada/mama”, pia anaweza kuiga, kuja aitwapo na kukubali kuvalishwa nguo

  • Mtoto mwenye miezi 18 anaweza kuonesha sehemu zake za mwili anapoulizwa, kucheza pekeyake

  • Mtoto mwenye miezi 24 anafuata amri, anaweza kutengeneza sentensi yenye maneno mawili

  • Mtoto mwenye miaka mitatu anaweza kutengeneza sentensi yenye maneno matatu, kutumia viwakilishi, kujua majina yake, pia anaweza kucheza na wenzake

  • Mtoto mwenye miaka minne anaweza kuongea vizuri kabisa na kueleweka, pia hucheza michezo ya vitu anavyo viwaza

  • Mtoto mwenye miaka mitano anaweza kuandika jina lake la kwanza, kucheza kwa kushirikiana na wenzake, kuelewa na kuzifuata sheria

Kumbuka.


Mtoto anaweza kufikia maendeleo yake ya ukuaji haraka au taratibu, hii hutegemea mazingira ya mtoto na lishe anayopata. Mtoto akipata lishe kama inavyoshauriwa kitaalamu ubongo wake utakuwa vema na hivyo kuweza kufikia maendeleo ya ukuwaji mapema zaidi kuliko watoto ambao hawapati lishe nzuri, wanauumwa umwa mara kwa mara, waliozaliwa na magonjwa au waliopata shida kipindi cha kuzaliwa. Hata hivo kuna baadhi ya mambo ambayo yanaweza kupelekea mtoto kupata maenedleo haraka haswa ya kuongea na kutembea haraka mfano mtoto anayekuwa na watoto wenzanke huwahi kutembea na kuongea kuliko mtoto ambaye hana mazingira kama haya. n.k

Elimu inayotolewa hapa ni kwa ajili ya ushauri tu na hivyo ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma makala hii.

Kwa ushauri zaidi na tiba, wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kupitia mawasiliano yetu

Imeboreshwa,

9 Novemba 2021 09:10:28

Rejea za mada hii:

  1. CDC.CDC’s Developmental Milestones.https://www.cdc.gov/ncbddd/actearly/milestones/index.html. Imechukuliwa 03.07.2020

  2. Medilineplus. Developmental milestone records. https://medlineplus.gov/ency/article/002002.htm. Imechukuliwa 03.05.2020

  3. Pathways.org. 0-3month milestone. https://pathways.org/growth-development/0-3-months/milestones/.Imechukuliwa 03.07.2020

  4. 3 to 6 months: Your baby's development. Zero to Three. https://www.zerotothree.org/resources/81-3-6-months-your-baby-s-development. Imechukuliwa 03.07.2020

bottom of page