Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, MD
9 Novemba 2021
Mtoto wa miaka 2 hadi 3
Maendeleo ya mtoto yakoje?
Kipindi hiki mtoto huwa na shauku ya kuwa huru, mtoto huwa ana fikra kubwa sana, huonesha mabadiliko ya kijamii kihisia na kitabia. Mabadiliko haya yatampelekea kutambua mambo mapya yanayomzunguka na kuyaelewa zaidi.
Anaweza kushika maagizo mawili hadi matatu katika hatua hii, mfano nenda kabatini kalete peni, kisha uje uniletee na maji ya kunywa.
Mtoto pia anaweza kupanga vitu vinavyofanana kulingana na rangi na umbo, huiga tabia za watu wakubwa na michezo na huwa na aina tofauti za hali.
Ukuji wa kimota
Mtoto mwenye miezi 24 anaweza kupanda na kushuka ngazi, kuchuchumaa na kusimama, kijivua nguo na kubebanisha vitu vitano hadi sita
Mtoto mwenye miaka mitatu anaweza kuendesha baiskeli ya magurudumu matatu, kurusha mpira mikononi na anaweza kuchora duara
Mambo ya kijamii, ufahamu, hisia na lugha
Mtoto mwenye miezi 24 anafuata amri, anaweza kutengeneza sentensi yenye maneno mawili
Mtoto mwenye miaka mitatu anaweza kutengeneza sentensi yenye maneno matatu, kutumia viwakilishi, kujua majina yake, pia anaweza kucheza na wenzake
Mambo ya kufanya
Vidokezo muhimu vya kulea mtoto kwa wakati huu
Vitu vifuatavyo mzazi unaweza kufanya ili kumsaidia mwanao katika maisha yake akue vema
Weka mdamaalumu wa kusoma vitabu vya watoto pamoja naye
Mhusishe na michezo mbalimbali
Msaidie mwanao atambue mazingira mapya na vitu kwa kumwacha acheze na kutembea sehemu sarama
Muulize mtoto jina lake na umri wake aseme
Mfundishe mwanao nyimbo rahisi za watoto
Wape umakini na wapongeze wakifuata maelekezo, punguza tabia ya kuangalia makosa na kumpa adhabu
Usalama wa mtoto
Kwa sababu mtoto hupenda kutembea tembea kwa wakati huu, usalama wake ni kitu cha kwanza. Fanya mambo yafuatayo ili kuhakikisha usalama wa mtoto wakati huu
Mshauri mtoto akae wakati wa kula na kutafuna chakula vizuri wakati wa kula ili kukinga kupaliwa
Angalia vifaa vyake vya kuchezea, hakikisha havijapasuka au kuvunjika, kama vimeharibika mtafutie vingine na hivyo vtupe ili asiumie
Msisitize asiweke kalamu au hela kwenye mdomo au pua
Usishike vinyaji vya moto wakati umempakata mwanao, mtoto anaweza kujitingisha na kuungua
hakikisha kama mtoto ameanza shule kwamba anapewa chakula chenye afya na vinywaji, na endapo wana mruhusu kuangalia Video na TV kwa kiasi
Mtoto anaweza kubadili nini cha kula kila mara, hii ni tabia ya kawaida si vema ukampiga au kumgombeza, mjaribishe kula vyakula vya aina tofauti vyanye afya hata kidogo kidogo
Usiweke TV kwenye chumba cha mtoto, mzuie mtoto asiangalie TV mara kwa mara wala kucheza game za kwenye TV, anaweza kuangalia TV kwa saa1 hadi 2 kwa siku
Mchagulie michezo ya kawaida kwa jinsi inavyowezekana, mtoto atakuwa kiakili na kuwa imara kiwmili kuliko kucheza game za kompyuta au kuangalia TV
Elimu inayotolewa hapa ni kwa ajili ya ushauri tu na hivyo ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma makala hii.
Kwa ushauri zaidi na tiba, wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kupitia mawasiliano yetu
Imeboreshwa,
9 Novemba 2021 09:00:24
Rejea za mada hii:
CDC.CDC’s Developmental Milestones.https://www.cdc.gov/ncbddd/actearly/milestones/index.html. Imechukuliwa 03.05.2020
Medilineplus. Developmental milestone records. https://medlineplus.gov/ency/article/002002.htm. Imechukuliwa 03.05.2020
Pathways.org. 0-3month milestone. https://pathways.org/growth-development/0-3-months/milestones/.Imechukuliwa 03.05.2020
3 to 6 months: Your baby's development. Zero to Three. https://www.zerotothree.org/resources/81-3-6-months-your-baby-s-development. Imechukuliwa 03.05.2020
Positive parenting tips for healthy child development: Infants (0-1 year old). Centers for Disease Control and Prevention. http://www.cdc.gov/ncbddd/childdevelopment/positiveparenting/infants.html. Imechukuliwa 03.05.2020