top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

9 Novemba 2021

Mtoto wa mwaka 1 hadi 2

Maendeleo ya ukuaji wa mtoto-Mtoto wa mwaka 1 hadi 2


Hatua zilizoelezewa hapa chini zimetokana na tafiti zilizofanywa na wanasayansi, hivyo zinatumika kama kipimo au rejea ya kusema mtoto wako ana maendeleo ya kawaida au yasiyo ya kawaida. Maendeleo ya mtoto yanapimwa kwenye vipengele vya mota, lugha


Vipimo vya ukuaji


Ukuaji wa mtoto huhusisha ukuaji wa uwezo wa kufanya kitu fulani ipasavyo, mfano kuanza kutambaa au kutembea kwa mara ya kwanza, kupunga mkono wa bye bye, kusema maneno na kuongea, anavyocheza, tabia yake, anavyoruka na kushirikiana na wenzake.


Ukuaji wa kimota


  • Mtoto mwenye mwaka mmoja(miezi 12) anaweza kutembea mwenyewe, kurusha vitu

  • Mtoto mwenye miezi 15 anaweza kutembea kinyume, kupanda ngazi, kuchorachora

  • Mtoto mwenye miezi 18 anaweza kukimbia kujilisha kwa kutumia kijiko kubebanisha vitu vinne

  • Mtoto mwenye miezi 24 anaweza kupanda na kushuka ngazi, kuchuchumaa na kusimama, kijivua nguo na kubebanisha vitu vitano hadi sita


Mambo ya kijamii, ufahamu, hisia na lugha)


  • Mtoto mwenye miezi 12 anaweza kutamka neno moja hadi manane tofauti na “dada/mama”, pia anaweza kuiga, kuja aitwapo na kukubali kuvalishwa nguo

  • Mtoto mwenye miezi 18 anaweza kuonesha sehemu zake za mwili anapoulizwa, kucheza pekeyake

  • Mtoto mwenye miezi 24 anafuata amri, anaweza kutengeneza sentensi yenye maneno mawili

Mwaka wa pili wa maisha


Mtoto huanza kujitambua na kutembea kwenda huku na kule kutokana na shauku ya kujua mambo na vitu vinavyomzunguka. Kwenye kipindi hiki mtoto anakuwa na tabia ya ubishi na asiyesikia mtu, kujitambua kwenye picha na kioo pia kuiga tabia za watu wengine wakubwa au watoto waliomzidi umri. Watoto wakati huu wanatakiwa pia kuweza kutambua majina ya vitu na wanafamilia anaoishi nao. Mtoto huweza kuongea sentesi fupi, kufuata maelekezo na miongozo wanayopewa. Mfano anaweza kuleta kitu kilicho ndani ya kabati mara baada ya kuambiwa niletee kitu fulani kipo ndani ya kabati.


Mambo ya kufanya

Mambo muhimu ya kukumbuka kuyafanya na yatamsaidia mtoto wako;


  • Msomee vitabu vinavyoendana na umri wake

  • Mwombe akutafutie kitu, au aseme majina ya sehemu ya mwili wako, mfano muoneshe mkono na aseme huo ni nini

  • Cheza michezo ya kutumia vifaa, mfano kupanga vitu vya watoto, kujenga nyumba ya kuunganisha vidude vya kujengea nyumba vya watoto, au kuunga puzzles n.k

  • Mwache acheze na kutambua mazingira yake vizuri na kujua mambo mapya

  • Msaidie mtoto kusema vema maneno ambayo hajui mfano akisema baba na akawa anaonyeshea chupa, mwambie ndio hii inaitwa chupa.

  • Mkuze kwa kujitegemea mfano kumsaidia anapovaa aingize mguu mwenyewe na mikono kwenye shati

  • Onya makosa ya kwa mtoto na kumwambia kwanini asifanye zaidi ya kumpa adhabu.mwambie anatakiwa kufanya nini mbadala

  • Mpeleke mtoto aka talii sehemu za wanyama au hata kutembea tu ili aweze kujua mazingira mapya na vitu vipya

Hakikisha usalama


Vitu vya kufanya ili kuhakikisha usalama wa mtoto


  • Usimwache mtoto karibu na majibila mtu kuwepo anayemwangalia wakati mtoto yupo kwenye maji. Hii inahusisha beseni au ndoo au bwawa la maji

  • Funga ngazi na mlango au kitu ili asipande maana anaweza Kupanda na kuanguka. Usimwache mtoto pia asiende maeneo ya matengenezo ya gari.

  • Weka vifaa vya moto mbali na mtoto, mfano pasi, hita ya maji n.k

  • Weka vitu vyenye ncha kali mbali na watoto ikiwa ni kisu, kiwembe au sindano na vitu vinavyoweza kumkata mtoto

  • Fungia dawa zote kabatini au weka sehemu ambayo mtoto hawezi kuzifikia kirahisi

  • Usimwache mwanao pekeyake kwenye gari hata kwa muda kidogo

  • Weka silaha zingine mbali nao ikiwa ni kisu, bunduki au bastola

Elimu inayotolewa hapa ni kwa ajili ya ushauri tu na hivyo ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma makala hii.

Kwa ushauri zaidi na tiba, wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kupitia mawasiliano yetu

Imeboreshwa,

9 Novemba 2021, 08:22:03

Rejea za mada hii:

  1. CDC.CDC’s Developmental Milestones.https://www.cdc.gov/ncbddd/actearly/milestones/index.html. Imechukuliwa 03.05.2020

  2. Medilineplus. Developmental milestone records. https://medlineplus.gov/ency/article/002002.htm. Imechukuliwa 03.05.2020

  3. Pathways.org. 0-3month  milestone. https://pathways.org/growth-development/0-3-months/milestones/.Imechukuliwa 03.05.2020

  4. 3 to 6 months: Your baby's development. Zero to Three. https://www.zerotothree.org/resources/81-3-6-months-your-baby-s-development. Imechukuliwa 03.05.2020

  5. Positive parenting tips for healthy child development: Infants (0-1 year old). Centers for Disease Control and Prevention. http://www.cdc.gov/ncbddd/childdevelopment/positiveparenting/infants.html. Imechukuliwa 03.05.2020

bottom of page