top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

9 Novemba 2021

Pozi la kunyonyesha mtoto

Unajua umuhimu wa kunyonyesha?

Maziwa ya mama huwa na kiwango sawia cha virutubisho na chakula anachotakiwa kupata mtoto. Maziwa ya mama ni rahisi kumengenywa kuliko maziwa mengine. Na maziwa ya mama huwa na kinga ya mwili kwa ajili ya kupambana na maradhi na hivyo huimarisha kinga ya mwili ya mtoto. Hata hiyo kunyonyesha kunaweza kukufanya upungue uzito na kupata faida nyingi . Tumia vidokezo hivi kujua uanzie wapi.

Kama umejifungua mtoto kwa mara ya kwanza inachukua siku 3 hadi nne ili maziwa yaanze kutoka, lakini kama umejifungua zaidi ya mara moja basi huweza kuchukua siku chache zaidi.


Siku zako za mwisho wa ujauzito yaani siku kadhaa kabla ya kujifungua, utahisi kuwa matiti yako yamejaa ikiwa ni dalili ya kuonyesha maziwa yanazalishwa.


Kiwango cha Homoni inayotoa taarifa kwamba maziwa yaanze kuzalishwa(prolactine) huongezeka kila sikukipindi chote cha ujauzito na hata hivyo huzuia kufanya kazi ipasavyo kutokana na homoni pingamizi zilizo katika kondo. Mara baada ya kujifungua homoni hii ya prolactin hufanya kazi ipasavyo na kuyaambia maziwa yatoke.


Maziwa ya kwanza ya mama huwa mazito nay a njano huitwa kwa jina jingine colostrums, maziwa haya huwa na kiwango kikubwa cha madini , protini, mafuta ambaya na kinga ya mwili.

Mara baada ya mtoto kuzaliwa anatakiwa kuwekwa kwenye ziwa ili apate kunyonya, labda uwe na tatizo ambalo umeshauriwa na daktari wako usimnyonyeshe.

Elimu inayotolewa hapa ni kwa ajili ya ushauri tu na hivyo ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma makala hii.

Kwa ushauri zaidi na tiba, wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kupitia mawasiliano yetu

Imeboreshwa,

9 Novemba 2021 12:35:32

bottom of page