top of page

Mwandishi:

Gamaliel K, CO

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

18 Novemba 2021

Udumavu

Udumavu ni nini?


Udumavu ni hali inayotokea wakati uwiano kati ya urefu na umri vinakuwa chini kwa vigezo vya ukuaji vilivyowekwa na shirika la afya duniani. kwa jina jingine udumavu unaweza kuelezewa kuwa ni udhaifu wa ukuaji wa mwili na maendeleo ya ukuaji wa mtoto unaotokea kwa mtoto kutokana na lishe duni, kuugua mara kwa mara na kukosa msisimuo wa kisaikolojia na kijamii.


Visababishi vya udumavu


  • Ulaji duni wa chakula kwa muda mrefu.

  • Magonjwa ya mara kwa mara.

  • Utapiamlo wakati wa ujauzito.

  • Upungufu wa nishati.


Tatizo hili la lishe husababishwa na kina mama kutopata mlo kamili wakati wa ujauzito. Tunaamini siku 1000 za kwanza wakati wa ujauzito ndicho kipindi ambacho uumbaji unafanyika, hivyo katika kipindi hicho mama akikosa kupata mlo kamili hupelekea mtoto kudumaa akiwa tumboni mwa mama yake.


Madhara ya udumavu


Madhara yanayojitokeza ni kama yafuatayo:-

  • Mtoto kudumaa kimwili, hii ni hali ya mtoto ambayo hupelekea mwonekano wake wa kimwili kuwa tofauti na umri wake, unaweza kukuta mtoto anamiaka mingi lakini umbo lake linakua dogo au anakua mfupi, kitaalam urefu unatakiwa kwenda sambamba na umri.

  • Mtoto kuwa na uwezo hafifu wa uwelewa na utambuzi wa mambo, hali hii hupelekea kuwa na wimbi la watoto mashuleni wasiofundishika.

Elimu inayotolewa hapa ni kwa ajili ya ushauri tu na hivyo ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma makala hii.

Kwa ushauri zaidi na tiba, wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kupitia mawasiliano yetu

Imeboreshwa,

18 Novemba 2021 06:41:54

Rejea za mada hii;

  1. Mafunzo ya lishe kwa ajili ya watoa huduma wa vituo - TFNC

  2. https://www.tfnc.go.tz › uploads › publications

bottom of page