Mwandishi:
ULY CLINIC
Wahariri:
Dkt. Sospeter B, MD, Gamaliel K, CO
18 Novemba 2021
Utapiamlo
Utapiamlo ni nini?
Utapiamlo ni hali ya kupungua au kuzidi kwa virutubishi mwilini inayosababishwa na lishe duni au lishe iliyozidi mahitaji ya mwili. Utapiamlo unaotokea sana Afrika hutokana na lishe duni.
Epidemiolojia ya tatizo
Utapiamlo husababisha vifo 300,000 vya watoto walio chini ya miaka 5kila mwaka katika nchi zinazoendelea, na pia huchangia zaidi ya nusu ya vifo vya watoto duniani
Lishe duni husababisha utapiamlo kuokana na kukosekana kwa virutubushi na husababisha kutokuwepo kwa usawa kati ya mahitaji ya chembe hai za mwili na virutubisho hivo kwa ajili ya ujenzi wa mwili(ukuaji), ulinzi wa mwili didi ya magonjwa n.k.
Mtoto mwenye utapiamlo huugua magonjwa kirahisi kutokana na kinga ya mwili kushuka na pia huwa na maendeleo hafifu ya kiakili na anaweza kupata matokeo mabaya ya kimaisha ya endapo hatapata tiba kwa sababu ya kudumaa akili na kushindwa kujishughulisha na pia ikumbukwe kuwa ni bora kujenga msingi imara ili kuweza kuhimili uzito wa ukuta utaosimama yaani maendeleo ya mtoto kiakili/afya bora huanzia utotoni
Aina za utapiamlo
Utapiamlo Mkali
Utapiamlo wa kadili
Dalili zipi za mtoto mwenye utapiamlo?
Utapiamlo unadalili mbalimbali na hutegemea nini kimepunguka mwilini kwa mtoto huyo. Dalili huweza kuwa;
Uzito chini ya kiwango/ kutoogezeka uzito au kuongezeka kidogo
Kutoongezeka urefu au kimo
Kwa watoto wadogo hubadilika tabia kwa kulia sana au kusumbua, kujitenga na wenzake au kutoshiriki michezo na watoto wenzake pia huwa na homu na kukosa umakini kwa mambo anayoyafanya
Dalili za utapiamlo kutokana na ukosefu wa viinirishe
Mtoto kama amekosa viinirishi huwa na dalili zifuatazo kutokana na kiinirishi alichokosa;
Kuchoka sana, kupungukiwa damu, hupungua kuelewa wa mambo anayofundishwa, kichwa kuuma na mabadiliko ya kucha- amepungukiwa madini chuma
Kuvimba kwa tezi ya thyroid, kuchelewa kukua, kupungua uwezo wa kiakili-mara nyingi huwa wamekosa madini joto
Kukua kwa shida, matege kwenye miguu--ukosefu wa madini ya calisium na virutubisho vya vitamini D
Kutoona usiku/kuona kwa shida wakai wa usiku, mabadiliko ya nywele- Ukosefu wa vitamini A
Ulimi kuuma/kupata michubuko, upungufu wa damu,tundu mgongoni--Mama alikosa madini ya folic acid wakati wa ujauzito
Kuwa mfupi, kuishiwa damu, bandama kuvimba, mabaka kwenye ngozi- Upungufu wa madini ya zinki
Dalili
Dalili anazoweza kuonesha mtoto kwa vipimo vya awali ni;
Kwa mwonekana ananekana amepungua mafuta chini ya ngozi hasamaeneo ya mikono,miguu, matakoni, na usoni
Kuvia maji kwenye miguu-(miguu kuvimba, uso au mwili mzima)
Kuchanika mdomo kwenye pembe, au ulimi kuchanika au ulimi kuwa mkubwa(kuvimba)
Tumbo kuvimba( mara nyingi Ini na bandama kuvimba husababisha hili)
Mabadiliko ya ngozi kama kupata mabaka na ngozi kubanduka kama maghamba ya mti, michubuko, mabaka meusi makubwa kwenye maeneo ya migandamizo
Hupata mabadiliko ya kucha
Nywele pia huwa dhoofu(nyepesi, kunyofoka kirahisi) na rangi ya mpauko au nyekundu
Uhusiano wa utapiamlo na maambukizi ya magonjwa
Lishe duni husababisha kushuka kwa kinga ya mwili na kupunguza uwezo wa mwili
kupambana na maambukizi hivyo kupata magonjwa kwa urahisi. Magonjwa yanaweza
kuathiri lishe kwa kupunguza hamu ya kula, kuongeza mahitaji ya virutubishi, kupotea kwavirutubishi na kuathiri ufyonzwaji wake mwilini. Hali hii inaathiri zaidi watoto wadogo kwa
sababu husababisha maendeleo duni ya ukuaji wa mwili na akili.
Vipimo gani mtoto anaweza kufanyiwa akiwa hospitali?
Kuna vipimo vya awali kinachofanywa na dakitari kwa kumchunguza au kumkagua mtoto na pia vipimo vingine vya kupima sukari mwilini na vipimo vingine vya kimaabara vinaweza kufanika kulinganana na mambo ambayo dakitari ameyaona na anataka kujihakikishia kwa vipimo kabla ya matibabu au baada ya matibabu
Elimu inayotolewa hapa ni kwa ajili ya ushauri tu na hivyo ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma makala hii.
Kwa ushauri zaidi na tiba, wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kupitia mawasiliano yetu
Imeboreshwa,
18 Novemba 2021 06:50:52
Rejea za mada hii
Mafunzo ya lishe kwa ajili ya watoa huduma wa vituo - TFNC
https://www.tfnc.go.tz › uploads › publications